
Na Baraka Mpenja,
Dar es salaam
Imechapishwa Agosti 1, 2014, saa 1:37 usiku
SIMBA SC
imewatambulisha wachezaji wawili iliyowasijili majira haya ya kiangazi kwa
mujibu wa mahitaji ya kocha mkuu, Mcroatia Zdravko Logarusic.
Makamu wa Rais wa
Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema zoezi la usajili linakwenda vizuri na
amewatambulisha Shaaban Kisiga `Malone` aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar na
Elias Maguri kutoka Ruvu Shooting.
“Zoezi la usajili
bado linaendelea kwa kuwa muda unaruhusu. Zoezi hili linaendelea kwa taratibu
na kwa umakini, wengine wanaweza kusema kuna ucheleweshaji au ugoigoi, usajili
ni jambo makini linalohitaji kufanywa kwa umakini mkubwa,” alisema Kaburu.
“Zoezi hili
linakwenda vizuri na kamati ya usajili inafanya kazi kwa ukaribu sana na benchi
la ufundi kupitia mwalimu wetu mku,”
“Na leo hii
tumekuja kuwatambulisha rasmi wachezaji wawili ambao simba imewasajili,”
“Mchezaji wa kwanza
ni Shaban Kisiga, uwezo wake mnaufahamu, ni mchezaji wa kimataifa, alishachezeaSimba
huko nyuma, akaenda kimataifa na akarudi Mtibwa na kusaini miaka miwili na sasa
anarudi nyumbani. Mchezaji wa pili ni Elias Maguri kutoka Ruvu Shooting”.
Baada ya
kutambulishwa, Shaaban Kisiga kwa apande wake alisema:
“Nashukuru kwa
kurudi klabu yangu ya Simba, nawashukuru viongozi na kocha. Nina imani
nitafanya vizuri na kuisaidia timu.”
Kwa upande wake
Maguri alisema: “Ninashukuru kujiunga na Simba, najua ni timu kubwa yenye
changamoto nyingi, kazi yangu sio kuongea bali ni vitendo uwanjani.”
Maguri amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Simba.
0 comments:
Post a Comment