
Na
Baraka Mpenja, kwa hisani ya mtandao wa Goal.com
Imechapishwa Agosti 1, 2014, saa 12:03 jioni
OSUMAR
SEIDU pengine alianza kuwaza kuwa anaelekea kutimiza ndoto zake za soka.
Alipanda
ndege mpaka nchini Urusi ambapo alifikiria kujiimarisha kama mchezaji wa soka
wa kimataifa, na labda siku moja aiwakilishe timu yake ya Taifa ya Ghana.
Kumbe
alikuwa amekosea sana. Alipewa uhakika wa kutimiza ndoto zake na jamaa mmoja aitwaye
Jermaine Owusu-huyu alidaiwa kuwa na leseni ya uwakala wa wachezaji ya FIFA
akifanya kazi na kampuni moja ya ‘Soccer Kick’.
Jamaa
huyu alisemekana kuwa anaishi mji mkuu wa Urusi, kwahiyo Seidu alianza kuhisi
ndoto zake za kutaka ufahari katika soka zinakaribia kutimia.
“Kitu
fulani kilienda ndivyo sivyo tangu mwanzo, ingawa sikuweza kujua ni nini kwa
wakati ule. Labda ilikuwa ni mipango iliyoshindikana,” anasema kijana huyo
mwenye miaka 23.
‘Mipango’
anayoisema kijana huyu ni ile ya Owusu kuchukua dola za kimarekani elfu 3000 (sawa
na milioni 4,800,000 za kitanzania) kwa ajili ya gharama za usafiri na malazi
wakati wote ambao Seidu atakuwepo Urusi.
Seidu
na mwenzake mwenye ndoto kama zake waliwasili Urusi wakiwa na matarajio makubwa
ya kufanya majaribio. Owusu alitegemewa kuungana na wachezaji hawa wawili
nchini Urusi muda mfupi ili kuona maendeleo yao kwenye klabu wanayotakiwa
kufanya majaribio.
Cha
kushangaza mambo yalikuwa tofauti na hatima yake ilikuwa ni nini?
Seidu
anasimullia kwa undani zaidi: “Baada ya kufika Moscow, tulipokelewa na Alhassan
mmoja, Mghana aliyehamia katika mji huo. Kwa
furaha alituchukua mpaka nyumbani kwake. Mwenzetu mmoja, anayeitwa Kojo,
alijiunga nasi baadaye. Cha kushangaza usiku, tuliambiwa tulipe dola mia 200
kwa ajili ya kodi ya nyumba na dola 100 kwa ajili ya kupata kibali cha kutembe
huru kwenye mji na dola zingine 50 kwa ajili ya chakula.
‘Mbaya
zaidi, Owusu hakuonekana mjini Moscow, licha ya kutuahidi kufika wiki moja tu
baada ya sisi kuwasili.”
Seidu
na rafiki yake waligundua kuwa mwenyeji wao, Alhassan ambaye aliigiza kuwa
mkarimu alikuwa muhuni na alishawahi kukaa jela nchini Urusi kwa miaka sita
kutokana na kumiliki dawa za kulevya kinyume na sheria.
Alishikiliwa
ndani ya ‘Obi manso’ (ardhi ya mtu mwingine). Seidu na rafiki yake wangehesabu
nini?
Wakala
aliyeonekana kuwa msaada, aliwatupa na kuwatupa kabisa? Je wameingia katika
mpango feki wa Owusu? Sasa wanafanyeje wakati wanaibiwa na watu ambao ni ndugu zao
kabisa?
Lakini
bado walikuwa wanahitaji kupata nafasi ya kucheza soka na walikuwa na matumaini
kuwa wakala wao atafika mjini Moscow.
“Baada
ya karibia mwezi mmoja kumalizika bila kwenda popote, rafiki mmoja wa Kojo
alitutembelea na kutupa mawasiliano ya watu wa michezo ambao wangekuwa msaada
kwetu.
“Bahati
nzuri, muda si mrefu tulijitambulisha kwa makocha wengi wa akademi za Urusi,”
Seidu anasimulia kwa tabasamu kidogo ingawa ni mazingira yanayoumiza.
Pale
walifurahia sababu yao ya kusafiri maili 4,042 kati ya Ghana na Urusi ambayo ni
kucheza mpira.

Seidu
anaendelea kusimulia, “ alitusafirisha sehemu nyingi kutafuta timu na alipata
klabu ya kujiunga mjini Dagestan (jimbo matata huko Urusi ambapo timu kubwa
yenye pesa ya Anzhi Makhachkala inapatikana), lakini ilishindikana kwasababu
Viza yangu ilikuwa imeisha muda siku nyingi,” anajaribu kukumbuka, lakini
anashindwa.
Seidu
na mwenzake wakafika pointi ya kuamini kuwa sasa Owusu amewaingiza
kichakani-mtu waliyemuamini sana na amewatupa kwenye ulimwengu wa huzuni na
masikitiko makubwa.
Hawakuwa
na sababu ya kuendelea kuishi kwenye Jimbo la Urusi wakiwa na nyaraka zilizoisha
muda wake. Wawili hao wakagundua njia pekee itakayowanusuru ni kutafuta namna
ya kurudi Ghana. Lakini kichwa kikawagonga, watapata wapi tiketi za ndege? Kumbuka
wametapeliwa fedha zao na Owusu.
Waliumiza
kichwa sana namna ya kupata tiketi za kurudi Ghana kutoka Urusi walipoamini
wangetimiza ndoto zao. Pia walihitaji kutumia kiasi fulani cha fedha kulipia
kibali cha kuishi nchini humo na fedha hizo zilichukuliwa na Owusu.
Mwenyeji
wao Alhassan akabadilika kuwa mbogo na kutaka kulipwa dola 200 kwa siku saba
zilizosalia, vinginevyo angewaacha mitaa ya Moscow ambapo ilikuwa rahisi
kupoteza maisha.
Seidu
na mwenzake, Afful, waligoma kulipa fedha hizo na kutafuta njia mbadala ambapo
waliamua kwenda ubalozi wa Ghana nchini Urusi ili kuomba msaada baada ya
kushindwa kutimiza mahitaji ya mtu mbaya Alhassan ambaye hakuwa na huruma kwa
ndugu zake na mhalifu mkubwa. Aliwanyonya kila senti waliyokuwa nayo.
SAFARI
YA KURUDI GHANA
Safari
iliandaliwa na ubalozi, tarehe ya kuondoka ilikuwa septemba 9, 2010, ambapo
Seidu anaikumbuka vizuri sana siku hiyo.
Baadaye
walitua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kotoka na walishangaa kukutana na Owusu
asiyekuwa na aibu uwanjani hapo. Seidu anakumbuka vizuri tukio hilo.
“Nilipandwa
na hasira, sikujisumbua kusemezana naye ingawa alionesha nia ya kutaka kuzungumza
nami, Mungu anajua zaidi,” Seidu anasema kwa uchungu.
Baada
ya kushindwa kuzungumza na kutokea ugomvi, mazungumzo yaliahirishwa mpaka siku
nyingine wakati ambapo hasira itakuwa imepungua. Seidu alienda ofisini kwa
Owusu akihitaji kurudishiwa kiasi fulaini cha fedha alicholipa kwa ajili ya
safari ya Urusi.
MATOKEO
YAKE ILIKUWA NINI?
“Hali
ilizidi kunichefua zaidi,” Seidu anasema. “Mara ya kwanza, aligoma kunipa
ninachodai.I linichukua mwezi mzima na hatimaye kupata changu. Hata hivyo
niliona kama ni fidia ya mateso niliyoyapa”.
“Uzoefu
alioupatakwa Owusu ulimfanya Seidu
alipeleke suala hilo kwenye vyombo vya habari na jeshi la polisi, mpaka sasa
jitihada zake zimegonga mwamba,”
FUNDISHO
KWA VIJANA
Ujumbe
unaopatikana hapa ni mwepesi sana, kiukweli: kama wewe ni kijana mdogo mwenye
kipaji cha soka na unahitaji nafasi ya kucheza nje ya nchi, pita njia sahihi na
usiwe na tamaa.
Usiongozwe na tamaa ya kupata mafanikio ya
haraka. Fuata taratibu zote. Usitake kuruka kwa haraka, utaingizwa kichakani
kama Seidu.
Hata
ukiona kwenye mitandao wanahitajika watu kama ilivyotokea kwa Seidu, kuwa mpole
na usijiingize kichwa kichwa ili kukwepa athari aliyoipata kijana huyu wa
Ghana.
0 comments:
Post a Comment