
Kiwango: Philippe Coutinho ameitwa kikosi ncha Brazil baada ya kuonesha kiwango kikubwa akiwa na Liverpool.
DUNGA ameanza majukumu yake ya ukocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil kwa mara ya pili kwa kuwapiga chini wachezaji 13 walioshiriki fainali za kombe la dunia.
Philippe Coutinho ni miongoni mwa wachezaji walioitwa kutokana na kiwango kizuri akiwa na Liverpool, wakati Neymar aliyepona majeruhi yake aliyopata katika fainali za kombe la dunia naye amejumuishwa katika kikosi hicho.
Kikosi cha wachezaji 22 kilitajwa jumanne kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Colombia na Ecuador.

Amerudi kazini: Dunga bado ina imani na Neymar katika michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Colombia na Ecuador.

Ametemwa: Wachezaji wengi wa kikosi kilichoshiriki kombe la dunia akiwemo Julio Cesar, wameachwa na Dunga.
Kipa wa QPR , Julio Cesar, beki wa kulia wa Barcelona Dani Alves, Marcelo wa Real Madrid na kiungo wa Tottenham, Paulinho ni miongoni mwa wachezaji wakubwa walioachwa katika kikosi hicho, wakati nahodha Thiago Silva amekosekana kutokana na majeruhi.
Dunga alimrithi Luiz Felipe Scolari baada ya kuvurunda katika fainali za kombe la dunia katika ardhi ya Brazil.
Brazil ilifungwa mabao 7-1 na Ujerumani, pia walifungwa mchezo wa mshindi wa tatu na Uholanzi.
0 comments:
Post a Comment