Mambo yatabadilika! Vincent Kompany amewapa hofu Liverpool katika kampeni za kuwania ubingwa.
NAHODHA wa Manchester, Vincent Kompany anaamini kuwa Liverpool watakabiliana na changamoto kubwa ya kuwania ubingwa tofauti na msimu uliopita kwasababu wana michuano ya ligi ya mabingwa.
Msimu uliopita, Liverpool walipewa nafasi ya kutwaa ubingwa wa kwanza ikiwa imepita miaka 24, lakini mwisho mwa msimu walizidiwa kete na Manchester City.
Timu hizo mbili zinakutana jumatatu ijayo katika mchezo wa ligi kuu England na wote walianza ligi kwa ushindi jumapili iliyopita.
Siku tatu baadaye timu hizi zitaingia katika makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Walizidiwa kete: Liverpool walikuwa na nafasi ya kutwaa 'ndoo', lakini walipigwa chini na Man City.
Kompany alisema: "Itakapokuja michuano ya ligi ya mabingwa itakuwa tofauti kabisa kwa Liverpool-kutokana na timu watakazokutana nazo hatua ya makundi. Wiki zitakuwa zinaenda na wanakabiliwa na michezo migumu kwa upande wa ligi na UEFA"
0 comments:
Post a Comment