Sunday, August 17, 2014

 Kocha wa Magolikipa wa Coastal Union, Meja akionesha matunda ya kazi yake ya kuwanoa makipa Mansour Alawi (kulia) na Fikirini Selemeni kushoto. Hii ilikuwa katika mechi ya ligi kuu dhidi ya Simba sc msimu uliopita uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo Wagosi wa Kaya walishinda bao 1-0


Na Mwandishi Wetu, Tanga


UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union “Wagosi Kaya “umekanusha vikali taarifa zilizizoenezwa kuwa mlinda mlando wa kikosi cha Vijana wenye umri chini ya miaka ishirikini U-20 Fikirini Suleimani “Mapara kuwa amesajiliwa na Klabu ya African Sports “Wana kimanumanu”

 Taarrifa hizo hazina ukweli wowote bali Fikirini bado ni mchezaji halali wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga na ni miongoni mwa wachezaji watakaoonekana kwenye kikosi hicho msimu ujao.

Taarifa iliyotolewa leo kwa nyombo vya Habari kupitia msemaji wa Klabu hiyo Oscar Assenga zimeelezwa kuwa fikirini bado ni mchezaji halali wa timu hiyo kwa kusajiliwa hivyo taarifa ya kuwa amejiunga na Africa Sports hazina ukweli wowote ule.

  Assenga amesema kuwa ili wadau wa soka waweze kuthibitisha kuwa mchezaji huyo bado yupo kwenye kikosi cha wagosi hao wa kaya wafike mazoezini Jumatatu kwani atakuwepo kwenye mazoezi hayo.

 Amesema kuwa Fikirini ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania bara.



0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video