Bado ipo moyoni: Suarez na Rodgers wakipongezana baada ya ushindi dhidi ya Norwich msimu uliopita.
BRENDAN Rodgers amefichua siri kuwa Luis Suarez alimtumia ujumbe mfupi wa simu akiitakia kila la kheri klabu yake ya zamani kuelekea mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu dhidi ya Southampton leo jumapili.
Wekundu wa Anfield walianza maisha ya ligi bila Suarez kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Muuruguay huyo aliondoka klabuni na kujiunga na Barcelona kwa dau la paundi milioni 75 majira haya ya kiangazi ya usajili.
Rodgers alisema mshambuliaji huyo alimtumia meseji nzuri ambayo aliijibu.
Rodgers alisema: 'Suarez alinitumia meseji nzuri asubuhi ya leo akitutakia kila la kheri na kuwaambia wachezaji wenzake wa zamani kuanza kwa nguvu. Ni rafiki wa Liverpool kwa sasa'
"Nilimjibu. Ni kijana mzuri, lakini ameondoka. Moyo wake upo Liverpool. Siku zote alitamani kukaa Liverpool na alimgusa sana'
Sturridge aliifungia Liverpool bao la ushindi na kuipa pointi tatu muhimu.
Akitoa maelekezo: Rodgers akiwaelekeza jambo wachezaji wake.
Magoli ya Raheem Sterling na Daniel Sturridge yaliipa ushindi Liverpool, wakati Nathaniel Clyne aliifungia Southampton bao la kusawazisha.

0 comments:
Post a Comment