
Imechapishwa Agosti 4, 2014, saa 3:30 usiku
TAARIFA zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa baraza la
vyama vya michezo kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati, CECAFA limekikataa
kikosi B cha klabu ya Yanya kilichopelewa
kushiriki michuano ya kombe la Kagame inayotarajia kuanza kushika kasi Agosti 8
mwaka huu, mjini Kigali, nchini Rwanda.
Imeelezwa kuwa Yanga wanatakiwa kubadilisha kikosi hicho
kufikia alfajiri ya kesho na kama haitafanya hivyo, basi timu itatolewa kwenye
mashindo.
Aidha, Taarifa hizo zinafafanua kuwa kama Yanga watashindwa
kutekeleza maamuzi hayo, basi mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc
watapewa nafasi hiyo.
Tangu awali CECAFA walisema Azam itapewa nafasi ya upendeleo,
lakini mpaka sasa wana Lambalamba hawajapewa taarifa rasmi.
Kocha wa Azam fc, Mcameroon, Joseph Marius Omog alisema kama
atapata nafasi ya Kombe la Kagame itakuwa nafasi nzuri ya kufanya maandalizi ya
ligi kuu na ligi ya mabingwa barani Afrika.
0 comments:
Post a Comment