
Imechapishwa Agosti 4, 2014, saa 5:43 usiku
TAARIFA Mpya usiku huu! Yanga hawatashiriki michuano ya klabu
bingwa kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati, maarufu kwa jina la Kombe la
Kagame inayotarajia kuanza kutimua vumbi Agosi 8 mwaka huu,, mjini Kigali,
Rwanda.
Hii imetokana na Yanga kugoma kubadili kikosi chao kama
walivyotakiwa na CECAFA leo hii.
Taarifa zinaeleza kuwa Yanga wamekomaa na kikosi B kama
walivyopanga wakati CECAFA wamewataka kwenda na kikosi B.
Awali ilielezwa kuwa Yanga
wanatakiwa kubadilisha kikosi hicho kufikia alfajiri ya kesho na kama haitafanya
hivyo, basi timu itatolewa kwenye mashindo.
Kwa mana hiyo, mabingwa wa ligi
kuu soka Tanzania bara, Azam fc wanaweza kupewa nafasi hiyo kama ilivyoelezwa
awali.
0 comments:
Post a Comment