Thursday, July 3, 2014

Yanga wameshaanza mazoezi chini ya kocha mkuu, Mbrazil Marcio Maximo

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976


Imechapishwa Julai 3, 2014, saa 2:39 asubuhi

MSIMU wa 2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania bara unatarajia kuanza kutimua vumbi mwezi agosti mwaka huu ambapo timu 14 zitachuana vikali kusaka taji linalomikiliwa na mabingwa Azam fc.

Ili kujiimarisha kwa ajili ya changamoto ya msimu mpya mpya, timu kadhaa zimeshaanza maandalizi ya kabla ya msimu `pre-sesson` wakiwemo Azam fc na Yanga sc.

Kama ilivyo kawaida, timu kubwa zimeshaanza mawindo, lakini baadhi ya timu zimelala usingizi wa `pono` mpaka sasa zikisubiri wiki mbili kabla ya ligi kuanza.

Maandilizi ya aina hii yanaitwa `zima moto`. Watu wa zima moto huwa wanakuwa na presha kubwa pale mambo yanapoanza kushika kasi. Kwa hali ya kawaida, sio rahisi kufanikiwa kutwaa ubingwa kwa kufanya maandalizi ya wiki mbili au tatu.

Unakumbuka msimu wa mwaka 2012/2013 Yanga walilazimika kuweka kambi ya wiki mbili nchini Uturuki na kufanikiwa kutwaa ubingwa. Msimu wa 2013/2014 walirudi tena Uturuki kwa  maandilizi ya mzunguko wa pili na ligi ya mabingwa.

Kwa kiasi kikubwa Yanga walifanikiwa, japokuwa huwezi kusema mambo ya Uturuki pekee ndio yaliwafanye wawe na makali dhidi ya Al Ahly, katika mechi mbili za ligi ya mabinga zilizopigwa Dar es salaam na Alexndria nchini Misri.

1471168_774363575937334_5147439689302321079_n
Watatetea ubingwa?: Azam fc ndio mabingwa watetezi wa ligi kuu, hivyo msimu ujao wana kibarua cha kulisaka taji hilo kwa mara ya pili pamoja na kuiwakilisha nchi katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika. 

Ikumbukwe katika safari  ya Azam fc, msimu wa 2012/2013 wao walienda kuweka kambi nchini Afrika kusini. Lakini msimu uliofuata hawakuweka kambi nje ya nchi, lakini waliendelea kujifua vikali katika uwanja wao wa kisasa wa Azam Complex uliopo Mbande, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. Maandilizi hayo yaliwafanya wafanikiwe kuwa mabingwa msimu wa 2013/2014.

Na kwa muda mrefu sasa wapo kambini kujiwinda na msimu mpya na tayari uongozi unasubiri kocha mkuu, Mcameroon, Joseph Marius Omog aweke wazi programu yake ya kambi ya nje ya  nchi.

Meneja wa Azam, Jamedari Said alisema jana kuwa uongozi unamsikiliza Omog na popote anapotaka kwenda kuweka kambi watamfanikishia safari na mambo yote ya kambi.

Huu ni ueledi wa uongozi wa Azam kwani wanatambua soka sio uchawi, bali ni maandalizi tu. Pia wanatambua mwakani wana kibarua cha ligi ya mabingwa baranI Afrika ambapo watakutana na miamba ya soka.

Wakati Azam fc ambao ni mabingwa watetezi wakiwa katika maandalizi, makamu bingwa Dar Young Africans, tayari nao wameshaanza mazoezi katika fukwe za koko beach na uwanja wa Bandari Tandika jijini Dar es salaam.

DSC_6109
Msimu ujao nani ataibuka kidume baina ya Logarusic wa Simba sc na Maximo wa Yanga?

Yanga wamekuja na nguvu mpya baada ya kumuajiri kocha Mbrazil, Marcio Maximo. Huyu ni kocha anayeufahamu utamaduni wa Tanzania kwani aliishi kutoka mwaka 2006 mpaka 2010 akiifundisha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Mbeya City fc walishika nafasi ya tatu msimu uliopita baada ya kukusanya pointi 49 katika mechi 26 walizocheza.

Ukiwa msimu wao wa kwanza, nafasi hiyo haikuwa mbaya kwao, lakini bila shaka wana mipango ya kuendeleza mafanikio hayo msimu ujao.

Mbeya City fc ni moja ya timu iliyochangia ligi kuu kuwa maarufu msimu uliopita. Kila kona ilikuwa gumzo na kila mpenda michezo alitamani kuona timu nyingine kama hii zinakuja ligi kuu.

Kwasasa wanasikika wakisema wamesitisha usajili kwasababu wachezaji waliopo wanatosha. Mbeya City bado hawajaanza programu rasmi ya mazoezi, ingawa  wanaendelea kujifua mdogo mdogo.

Simba walioshika nafasi ya nne kwa kujikusanyia pointi 38 wao wametoka katika hekaheka za uchaguzi, hivyo haijawa rahisi kwao kuanza maandalizi kama ilivyo kwa wapinzani wake Yanga, Azam fc na Mbeya City.

Evans Eliaza Aveva amechaguliwa kuwa rais wa kwanza wa klabu hiyo. Huyu ni moja ya watu wa `Friends of Simba`. Hili ni kundi lenye nguvu zaidi katika klabu hiyo.

3604702_orig
Watamzuia Mnyama tena?: Simba walimaliza nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City nafasi ya tatu. Logarusic na bosi wake Aveva watakubali msimu ujao? 

Ushindi wake unatafsiriwa kurejesha nguvu ya mamilionea hawa wa Friends of Simba ( F.O.S) mitaa ya Msimbazi. Aveva alimwaga sera safi kabisa ikiwemo kufanya usajili wa nguvu ili kuirejesha klabu hiyo kwenye soka la ushindani.

Sasa yametimia na alishinda kwa kishindi, watu wanasubiri usajili wa haraka ili waanze maandalizi chini ya kocha wao mkuu, Mcroatia, Dravko Logarusic.

Uzuri ni kwamba mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alisema tayari wameshafikia mazungumzo na wachezaji wanaowahitaji, lakini alikataa kuwapa mikataba mpaka watakapopatikana viongozi wapya. Zoezi hilo limekamilika na bila shaka majina yataanza kuanikwa na kuona picha za wachezaji wakisaini mikataba mipya, japokuwa kuna wameshafanya kwa mmoja

Ukiziangalia timu zilizoshika nafasi nne za juu, Azam fc, Yanga, Mbeya City na Simba sc. Unaona zina nia ya kuendeleza mafanikio ya msimu uliopita au kuzidisha zaidi.

Azam watakuwa na kibarua cha kutetea ubingwa, Yanga watakuwa na kibarua cha kurejesha taji jangwani, Mbeya City fc watakuwa na kibarua cha kusaka ubingwa, Simba watakuwa na kibarua cha kurudisha heshima kwa kutwaa ubingwa.

Kutokana na mazingira haya, ni rahisi kusikia timu hizi zikianza maandalizi mapema.

Ruvu Shooting walishika nafasi ya sita kwa kujikusanyia pointi 38 nyuma ya Kagera Sugar.

Klabu hii inayonolewa na kocha Mkenya Tom Alex Olaba ilishaanza maandalizi ya msimu mpya na umekamilisha usajili wa wachezaji watano wapya. Shooting inaonekana kujipanga na kuwa na nidhamu ya mpira. Maandilizi ni muhimu katika mchezo wa soka.

Lakini kuna timu ambazo hazikufanya vizuri kutokana na uzoefu wao, lakini zimekaa kimya. Labda zinafanya mambo kimya kimya, lakini sidhani kama zipo katika maandalizi `bab kubwa`.

_DSC0696
Mtakuja na jipya?: Simba hii haikufanya vizuri msimu uliopita.

Wapi Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons, Coastal Union, Mgambo JKT?. Binafsi nilitegemea kusikia maandalizi ya nguvu kwa timu hizi kutoka na matokeo ya `kuungaunga` waliyopata msimu uliopita, lakini imekuwa tofauti.

Yawezekana baadhi ya timu hizo zina tatizo la uchumi, lakini nyingine sidhani kama zina tatizo hilo. Kinachoonekana ni kukosa mipango.

Timu nyingi zina malengo ya kushiriki ligi kuu na si kushindana. Malengo yao yanakuwa kubaki ligi kuu tu, lakini mambo mengine kama kusaka ubingwa hawana muda  kufikiria.

Ili kupata ligi bora zaidi ya msimu uliopita, ingekuwa bora kwa timu zote kuanza maandalizi ya mapema. Nasikia habari za Ndanda fc, Stand United na Polisi Morogoro.

Hizi ni timu mpya. Naambiwa zimeshaanza maandalizi na zinazionya timu zilikuwepo msimu uliopita. Sina hakika zitakuja kwa kasi ipi, lakini naamini zimejipanga vizuri.

Viongozi wa timu za ligi kuu maandalizi ya mapema ni mazuri sana. Kuna njia nyingi za kuiandaa timu hata kama huna hela.

Kumbuka kufanya vizuri kunaleta udhamini. Hamuoni milioni 360 za Bin Slum katika klabu ya Mbeya City fc?, ni matunda ya kufanya vizuri.

Hata kama hamna hela ya kutosha kuweka kambi, tumieni utaratibu wa wachezaji kutoka majumbani kwao na kufanya mazoezi ya nguvu pamoja.

Sibezi maandalizi ya timu yoyote, lakini nakumbusha kuwa kila jambo linaanza na maandilizi bora.


Kila la heri timu za ligi kuu soka Tanzania bara kuelekea msimu mpya wa wa 2014/2015 unaotarajia kuanza kushika kasi mwezi agosti mwaka huu.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video