Thursday, July 3, 2014

IMG_0080
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam


Imechapishwa Julai 3, 2014, saa 2:09 asubuhi

WASHINDI wa tatu wa ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita, Mbeya City fc wamesitisha suala la usajili wa wachezaj kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu unaotarajia kuanza mwezi Agosti mwaka huu.

Katibu mkuu wa klabu hiyo, Emmanuel Kimbe amesema wamefanikiwa kusajili wachezaji watatu tu kama alivyoelekeza kocha mkuu, Juma Mwambusi.

“Kikubwa ni kwamba, sisi katika suala la usajili, hatujasajili wachezaji wengi sana. Tumesajili wachezaji watatu tu na tumemaliza usajili kwa upande wetu. Katika idadi hiyo ya wachezaji, yupo Them Felix kutoka Kagera Sugar”. Alisema Kimbe.

Kimbe aliongeza kuwa wachezaji hao watatu wanatosha na sasa wanaelekeza nguvu kubwa katika timu yao ya pili itakayosaidia kujenga timu ya wakubwa.

“Tumefanya kwa mahitaji kwasasa. Wachezaji wetu wengi wapo, kwahiyo hatukuona sababu ya kujaza wachezaji ambao hatutawatumia. Kwanza unawakosea, unawatumia chini ya asimilimia 10, si jambo zuri”.

1e
“Tuna wachezaji wanaoweza kutumika vizuri kwa mujibu wa mahitaji ya mwalimu. Kwa nafasi alizopendekeza, tumefanyia kazi, na maeneo mengine yapo vziuri”. Aliongeza Kimbe.

Hata hivyo Kimbe aliwataka wapenzi wa Mbeya City fc kutulia kwasababu wana mkakati mzito wa kufanya mabadiliko ndani ya klabu.

Alifafanua kuwa wapo watu mikataba yao imeshamalizika, huku wengine wakiongezewa na wengine hawataongezewa.

“Kila kitu tunachofanya ni kuifanya klabu kuwa ya kisasa. Kuna mabadiliko ya kiuongozi, benchi la ufundi na wachezaji, lengo ni zuri tu”. Alieleza Kimbe.

Siku chache zilizopita, aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo, Maka Mwalwisyi alitangaza kuachana na klabu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika mwezi mei mwaka huu.

Maka alieleza kuwa aliamua kuachana na Mbeya city fc ili kupata changamoto mpya hasa baada ya kupata kozi ya leseni B ya CAF iliyofanyika jijini Dar es salaam.


Kocha huyo muumini wa soka la vijana alisema sasa anahitaji kupata timu ya kuwa kocha mkuu ili aitambulishe falsafa yake tofauti na alipokuwa anafanya kazi chini ya falsafa ya bosi wake, Juma Mwambusi.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video