
Timu ya Taifa (Taifa Stars) imevurumishwa
mabao 4-2 katika mechi ya kirafiki na Botswana jana.
Mechi hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Gaborone ni
sehemu ya maandalizi ya Taifa Stars kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika
dhidi ya Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Mabao ya Taifa Stars yalifungwa na Khamis
Mcha `Vialli` na nahodha wa Azam fc, John Raphael Bocco `Adebayor`
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager inatarajiwa kurejea nchini Julai 6 mwaka huu kuendelea na
programu nyingine kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji.
0 comments:
Post a Comment