
Wachezaji
wa Young Africans wakiwa mazoezini jana asubuhi Coco Beach
Na
Baraka Mpenja, Dar e salaam
MAKAMU
bingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu uliopita, Dar Young Africans
imeanza mawindo ya msimu ujao unaotarajia kuanza mwezi agosti mwaka huu chini
ya kocha mpya Mbrazil, Marcio Maximo.
Maximo
mwenye heshima kubwa nchini baada ya kuiongoza Taifa stars miaka minne
iliyopita aliongoza mazoezi ya Yanga kwa mara ya kwanza jana katika Ufukwe wa Koko Beach.
Katika
mazoezi hayo, jumla ya wachezaji 14 kutoka timu ya wakubwa walihudhuria na kufanya
mazoezi ya kusaka pumzi na kujenga mwili.
Wachezaji
waliofanya mazoezi chini ya Maximo mwenye msimamo wa falsafa yake na nidhamu ni
Ally Mustafa "Barthez" , Juma Abdul, Swaleh Abdallah, Rajab
Zahir, Mbuyu Twite, Salum Telela, Omega
Seme, Hassan Dilunga, Said Bahanuzi, Andrey Coutinho, Hussein Javu, Juma
Kaseja, Nizar Khalfani, na Jerson Tegete.
Katika
mazoezi ya jana Maximo aliendelea kuwakosa wachezaji 11 ambao wapo katika timu
za Taifa wakijiandaa na mechi za mwishoni mwa mwezi huu kusaka tiketi ya
kushiriki fainali za mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.
Wachezaji
walio kwenye timu ya Taifa Tanzania ni Deo Munish "Dida", Oscar
Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub "Cannavaro", Saimon Msuva,
Mrisho Ngasa, Pato Ngonyani, Said Juma
huku Uganda ikiwa na Emmanuel Okwi, na Hamis Kizza na Rwanda Haruna Niyonzima.
Countinho
aliyesajiliwa kutoka nchini Brazil alitazamwa kwa mara ya kwanza na baadhi ya
mashabiki waliojitokeza katika mazoezi hayo.
Jana
jioni Yanga iliendelea na mazoezi yake katika uwanja wa Bandari uliopo Tandika
jijini Dar es salaam.
Maximo
anatarajia kuleta mafanikio katika klabu yake ya Yanga hasa kuboresha mfumo wa
soka la vijana.
Enzi
zake akiwa Taifa stars, Mbrazil huyu aliinua vipaji vya wachezaji vijana
wakiwemo Jeryson Tegete na Kigi Makassi.
Maximo
alisema nia yake ni kuifanya Yanga kuwa tishia Tanzania na barani Afrika.
0 comments:
Post a Comment