Saturday, July 5, 2014

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

Imechapishwa Julai 5, 2014, saa 4:42 asubuhi

BAADA ya mapumziko ya kutoona mechi za ligi kuu katika dimba la Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya, wapenzi wa soka leo hii watajikumbushia ladha ya soka kwa kuzishuhudia Mbeya City fc na Tanzania Prisons zikichuana vikali.


Hii ni mechi maalum ya kajaribu mfumo wa tiketi za elekroniki katika dimba hilo na inatarajia kuanza majira ya saa 10 kamili jioni.


Mbali na kuwa mechi ya kirafiki, pia itatoa fursa kwa wapenzi wa timu hizi kuona vikosi vyao wakati huu maandalizi ya ligi kuu soka Tanzania bara yakiendelea kushika kasi.


Shirikisho la soka Tanzania, TFF, lilitangaza kiingilio cha mechi hiyo kuwa ni shilingi elfu tatu kwa majukwaa yote ambapo tiketi zilianza kuuzwa julai mosi mwaka huu kupitia M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka ya Fahari Huduma.


 Wakati huo huo, jana, julai 4 mwaka huu, shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liliendesha mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki kwa wadau wa mpira wa miguu mkoani Mbeya.

Mafunzo hayo yalifanyika kwenye Uwanja wa Sokoine, na kushirikisha wasimamizi wa mechi, viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA) na makatibu na maofisa habari wa klabu za Tanzania Prisons na Mbeya City.



Wengine walioshiriki mafunzo hayo ni Meneja wa Uwanja wa Sokoine na msaidizi wake, wasimamizi wa milangoni (stewards) na waandishi wa habari wa mkoani Mbeya.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video