
Mshambuliaji Brain Umony (kushoto) ameachwa na Azam fc
Na Baraka Mpenja Dar es salaam
Imechapishwa Julai 5, 2014, saa 3:30 asubuhi
MABINGWA wa soka Tanzania bara, wana Lambalamba Azam
fc wamevunja mkataba na mshambuliaji wao raia wa Uganda, Brian Umony.
Umony hayupo kwenye mipango ya kocha mkuu wa klabu
hiyo, Mcameroon, Joseph Marius Omog, hivyo uongozi umelazimika kuachana naye.
Afisa habari wa klabu hiyo, Jafar Idd Maganga
amesema Umony baada ya kuitumikia Azam kwa mwaka mmoja na nusu ama miwili, wameamua
kuachana naye kwa amani na kumpati stahiki zake.
“Uongozi wa Azam umekaa na mchezaji huyo na
kuvunja mkataba wake. Kwa maana hiyo amepata stahiki zake na amekwenda mbele
katika maisha yake ya mpira”. Alisema
Jafar.
“Ni kawaida
kwenye mpira kuwa, yule anayesitishiwa
mkataba wake anatakiwa apewe haki yake. Wengine wanamuacha halafu hawampi haki
yake na ndio maana unaona mchezaji anakwenda kushitaki TFF au FIFA. Sisi
tunamwambia mchezaji, tunakaa naye na tunakubaliana na kumpa haki yake”.
Hata hivyo, Jafar alisema wana nafasi moja ya
kusajili mchezaji mmoja wa kimataifa na kama watapata kifaa kipya basi
watafanya hivyo, japokuwa sio lazima kumaliza nafasi zote.
Afisa habari huyo alisema kikosi chao kinaendelea
vizuri na maandalizi ya ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajia kuanza kushika
kasi mwezi agosti mwaka huu pamoja na ligi ya mabingwa barani Afrika.

0 comments:
Post a Comment