
Kocha Marcio Maximo akiwa na msaidizi wake Leonardo Neiva
Kocha mkuu wa timu ya Young Africans SC Mbrazil
Marcio Maximo amesema atakua akiongea na waandishi wa habari kila siku ya
Ijumaa asubuhi mara tu baada ya mazoezi katika shule ya sekondari Loyola ili
kuwapa nafasi na fursa ya kumuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na maandalizi
ya kikosi chake msimu ujao.
Akiongea na mtandao rasmi wa klabu ya Young
Africans Maximo amesema, ameamua kufanya hivyo ili kupunguza kuwepo taarifa
tofauti kuhusiana na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wake katika
maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015.
“Unajua utendaji wa kazi umebadilika, nafasi yangu
kwenye klabu na nilipokua timu ya Taifa ni tofauti, hivyo nimekubaliana na
uongozi na umeniruhusu kuwa naongea na vyombo vya habari kwa pamoja kila siku
ya Ijumaa mara tu baada ya mazoezi ya asubuhi "alisema Maximo"
Waandishi wa habari, Vyombo vya Habari mnaombwa
kuhudhuria kila siku ya ijumaa shule ya sekondari Loyola ili mpate nafasi ya
kuongea na kocha Maximo na kumuuliza maswali, kwani kwa sasa yeye ndie
atakayekua akiongelea timu, wachezaji pamoja na benchi lake la ufundi.
Maximo ameanza kazi ya kukinoa kikosi cha
Young Africans tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na kuwatuvia wapenzi, washabik
na wanachama ambao wamekua wakijitokeza kwa wingi kushuhudia ufundishaji wa
kocha huyo mwenye mvuto mkubwa kwenye soka la Tanzania.

0 comments:
Post a Comment