Oliver Bierhoff, wa pili kutoka kushoto, aliifungia bao la kwanza timu yake katika fainali za Euro za mwaka 1996 kati ya Ujerumani na Jamhuri ya Czech, moja ya kombe la karibu la kimataifa ambalo Ujerumani wameshinda.
Oliver Bierhoff anajua
jinsi ya kushinda kombe. Mshambuliaji huyo wa zamani wa AC Milan mwenye miaka
46 aliifungia goli la ushindi Ujerumani katika fainali za Euro za mwaka 1996
kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Czech Republic ndani ya uwanja wa Wembley.
Bierhoff, meneja mkuu wa
timu ya taifa ya Ujerumani, ametumia muda wake kuongea kwa njia ya simu na
mtandao wa ESPN FC akizungumzia mchezo wa nusu fainali wa usiku dhidi ya wenyeji
Brazil, hususani akizungumzia nafasi ya Ujerumani na jinsi watakavyotumia
teknolojia kuwafunga wapinzani wao.
Raphael Honigstein: Mr. Bierhoff, vipi morali ya kambi
kuelekea mchezo wa nusu fainali dhidi ya Brazil Brazil?
Oliver Bierhoff: Timu iko imara, timu iko tayari. Nimekuwepo kwenye
mashindano mengi, kama mchezaji na meneja mkuu, lakini sijawahi kuona timu
ambayo inashangilia kidogo baada ya kushinda robo fainali. Kwa asilimia kubwa
wana malengo, hawataki safari kufika mwisho. Nadhani safari ya Rio (kwa ajili
ya mchezo wa Ufaransa) pia ilisaidia kwasababu nilimpa kila mchezaji majukumu
kuwa tunatakiwa kufika fainali Maracana. Utulivu umekuwa mkubwa, lakini kuna
hali ya ugumu wa mchezo kidogo.
RH: Hakuna anayetaka kucheza
mechi ya mshindi wa tatu. Je, kombe la dunia mwaka huu litapimwa kama mafanikio
ya Ujerumani hata kama hawatafika fainali?
OB: Kwangu mimi , ndiyo.
Tunataka kushinda kombe kwa gharama yoyote. Lakini kitu chochote kinaweza
kutokea katika mchezo wa nusu fainali au fainali. Unaweza kuwa katika kiwango
chako kikubwa na bado ukapoteza. Au unaweza kushinda kwa bahati. Tofauti ya
timu hizi mbili ni ndogo. Yote kwa yote, ninachoweza kusema wachezaji kwa kweli
wanahitaji kushinda kombe.
RH: Unautazamaje mchezo dhidi
ya Brazil?
OB: Watakuwa
wapinzani wagumu, hata kama hawana Neymar na Thiago Silva. Watacheza pamoja
kama timu. Wataalam wetu wameitazama Brazil kwa miaka minne. Tuna data kutoka
kwenye michezo yao bila Silva na Neymar. Tumewaonesha vijana wetu namna ya
kuwashinda Brazil.
Tumefanya maarifa na kuweka
takwimu hizi katika simu. Data zinapatikana kirahisi na wanajua ni mchezaji
gani atakuwa mshambuliaji badala ya Neymar, kwa mfano tunaweza kuwaambia mabeki
juu ya wachezaji wawili au watatu wanaoweza kumbadili. Hii imetusaidia sana.
RH: Unaweza kutupa mfano
mwingine jinsi ambavyo wachambuzi wa mpira wanatumiwa na timu ya Ujerumani
nchini Brazil?
OB: Tuligundua kuwa
wachezaji wanapenda kuwasiliana kwa vifaa vyao vya kiteknolojia. Kwahiyo kwa
msaada wa wataalam wetu wa teknolojia, tulikuja na mfumo ambao unatusaidia
kutupa vipande vya video za uchambuzi kwa mchezaji mmoja mmoja au makundi ya
wachezaji kutoka timu mbalimbali. Kila mchezaji anapata mifano mingi ya jinsi
alivyocheza vabaya na vizuri baada ya mechi. Wanaweza kutazama kwa muda wao na
kuangalia takwimu za viwango vyao. Hii imetusaidia sana kuliko kuonesha mkanda
wa video wa dakika 90. Wachezaji wanafurahia hali hii na wanatoa mrejesho
mzuri.Pia tuna takwimu mbalimbali za wapinzani wetu. Jérôme Boateng aliombwa
kumtazama Cristiano Ronaldo jinsi anavyotembea akiwa katika eneo la boksi, huo
ni mfano mwingine. Na kabla ya mchezo dhidi ya Ufaransa, tuliwaona Ufaransa
wakiwa watulivu eneo la kiungo, lakini maeneo ya pembeni yalikuwa na udhaifu
kwasababu mabeki wao wa pembeni walikuwa hawapandi vizuri. Kwahiyo tulitumia
nafasi hizo.
RH: Je, mnajiamini tangu muwafunge Ufaransa?,
ukitazama matokeo ya 2-1 dhidi ya Algeria pia yaliibua wasiwasi mkubwa.
OB: Wasiwasi huu ulizushwa nje
ya kambi, lakini ndani ya kambi hakuna tatizo. Moja ya kazi yangu ni kuwapa
moyo wachezaji. Huwezi kuruhusu hisia za hofu zikaja karibu yako, hususani
kutoka nje ya timu. Baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Ureno katika mchezo
wa ufunguzi. Nilitoa ruhusa ya kupiga simu kwa yeyote anayetaka kujadili kwa
namba gani tunaweza kushinda kombe la dunia. Siku kadhaa baadaye, baada ya sare
ya 2-2 na Ghana, kila mtu alikuwa na wasiwasi. Maneno haya yalikuwa na athari
na yalitufanya tubadilike kila mchezo. Huwezi kujitenga kutokana na haya.
Tumeweza kufanya vizuri, kwa mtazamo wangu. Na wakati mwingine, nimekuwa
nikiwaambia wachezaji: Huu ni mchezo—huu ni mchezo.

0 comments:
Post a Comment