Wednesday, July 9, 2014


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

0712461976


Imechapishwa Julai 9, 2014 saa 3:53 asubuhi

LUIZ Felipe Scolari amekubali kubeba lawama zote kutokana na fedheha waliyoipata Brazil kutoka kwa `watu katili` Ujerumani.

Haikutegemewa na wengi kama Brazil wangeingia katika rekodi mbaya ya kombe la dunia kwa kufungwa mabao 7-1 na Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia jana usiku.

Brazil waliojiamini, waliingia kwa kasi, lakini bao la mapema la Thomas Muller liliwatoa upepo ghafla ya kufungisha mabao mengi zaidi.

Bora Neymar hakuwepo katika mchezo huo. Huyu ni mchezaji mwenye kiwango cha juu kama alivyo kwa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Kama angekuwepo uwanjani, halafu Brazil ikafungwa mabao kama ya jana, basi ingemharibu zaidi katika maisha yake ya soka.

Tatizo kubwa la Brazil lilikuwa kwenye safu ya ulinzi iliyoongozwa na nahodha David Luiz, Maicon, Marcelo na Dante. Hawa walikuwa tatizo jana, walikaba vibaya, utulivu ulikuwa `F`. Hata Neymar angekuwepo, kwa aina ya uchezaji wake, bado safari ya Brazil ingefika mwisho kwasababu asingekuwa na jinsi ya kuwaokoa.

Emotional: David Luiz unable to hold back the tears following full time
Mambo ya `wedi kapu` haya, si mchezo: David Luiz alishindwa kuzuia machozi baada ya `mbungi` kumalizika.

Pole sana Scolari, pole sana Neymar, Pole sana Thiago Silva, pole sana wananchi wa Brazil, pole sana mashabiki wa Brazil duniani kote. Huo ndio mpira wa miguu, Rekodi yenu itazungumzwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Hongereni Ujerumani kwa ushindi mnono. Hongereni kwa Miroslav Klose kuvunja rekodi ya gwiji wa Brazil, Ronaldo. Mabao 16 na kuwa mfalme wa mabao wa kombe la dunia ni heshima kubwa.

Kwa umri wa miaka 36, kwa watu wengine wangeona hustahili kuingia kikosi cha Ujerumani kilichosheheni nyota wengi. Lakini kwa kutambua umuhimu wa rekodi, mlimchukua ili atimize malengo yake. Klose ameheshimiwa na kupewa nafasi, na mwisho kafikia malengo. Hongera Mkongwe.

Distraught: Brazil fans at the stadium in Belo Horizonte stand in disbelief
Jukwaani nako kulikuwa na majanga, Mjerumani `Katili` sana 

Dunia ilisimama kwa dakika 90 jana, shughuli zilisimama kushuhudia nini kimewakumba mabingwa hao mara tano wa dunia.

Wakati kocha Scolari akiumiza kichwa jana, kwa upande wa makocha wa Simba sc, mambo yanatakiwa kuendelea kama kawaida.

Kocha msaidizi wa Simba, Seleman Abdallah Matola anatarajia kuanza kuiongoza klabu hiyo katika mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu kuanzia leo julai 19, 2014 kwenye uwanja wa Boko Veteran uliopo Boko.

Matola ataanza majukumu hayo wakati huu ambao kocha mkuu wa klabu hiyo, Mcroatia Dravko Logarusic hajawasili nchini.

Kwa taarifa za ndani ya Simba sc, Loga anaweza kuwasili kesho alhamisi na  ijumaa kujiunga na Matola kuendeleza gurudumu la maandalizi.

Huu ni wakati mwingine muhimu kwa Simba. Wanahitaji kuwaunga mkono makocha wao, wachezaji wao ili waiendeleze klabu hii.

Kwa miaka mitatu sasa, Simba imekuwa akiwaumiza mashabiki wake. Matokeo yake yamekuwa ya kuungaunga tu, hivyo kuna ulazima kwa kila mwanasimba kutoa mchango wake kwa nafasi aliyonayo.

_DSC0659
Kocha Mkuu wa Simba sc, Mcroatia, Dravko Logarusic (wa kwanza kushoto) ana kazi ya kuijenga klabu hiyo.

Makocha kazi yao ni kufundisha mbinu za uwanjani,ufundi wa kucheza mpira,  kuwajenga wachezaji kisaikolojia na mengine ya kitaalam. Ili kufanya kazi hii lazima uwe na taaluma.

Loga na Matola wana nafasi ya kukaa na wachezaji kwa muda mwingi kuliko mtu yeyote. Wao ndio wanajua nani mzuri nani mbaya. Wao wanajua nidhamu ya mchezaji mmoja mmoja.

Kwa kifupi, masuala yote ya kitaalam ya uwanjani, wao ndio mabosi. Hapa hakuna wa kuingilia, kama ikitokea mtu wa nje na benchi la ufundi kaingilia, ujue ndio siasa za Simba na Yanga hizo, pamoja na timu za majeshi.

Cha msingi, makocha waachwe wafanye kazi kwa kuzingatia ueledi wao. Anachoweza kufanya mtu wa nje, ni kushauri tu, tena sio lazima ushauri uchukuliwe.

Benchi kama sehemu ya kwanza ya timu, liachwe lifanye kazi yake ili malengo ya kuijenga timu yatimie. Wanasimba, waungeni mkono Loga na Matola ili wawarudishe katika hadhi yenu.

_DSC0696
Sehemu nyingine muhimu katika kuijenga Simba sc, ni wachezaji wenyewe.

Wanandinga wa Simba lazima mjue kuwa kuna watu wengi nyuma yenu. Fanyeni kazi yenu kwa bidii. Nidhamu ni kitu cha msingi. Maandalizi mazuri yatawapa matokeo mazuri.

Zingatieni maelekezo ya makocha na kuongezea akili zenu.Hamuwezi kufundishwa kila kitu, jifunzeni mbinu mpya ili muisaidia Simba.

Mchango wa viongozi chini ya Rais, Evans Aveva, ni kusaidia mambo ya kiutawala. Wao wana wajibu wa kuhakikisha mambo yote ya kambi, mazoezi, mishahara,posho na mengine yanayohitaji fedha yanafanyika kwa wakati.

Watanzania tunajijua maisha yetu. Bila kupewa kichache cha mfukoni, kazi inalala, na hii inatokana na kutegemewa zaidi pale unapokuwa na hela.

Baadhi ya wachezaji wanasomesha, wana familia, wanategemewa na watu tofauti tofauti,  hivyo kuwacheleweshea posho na mishahara, unawaondolea ufanisi wa kazi.

Big Bosi: Rais wa Simba sc, Evans Elieza Aveva

Aveva jukumu lako ni kumaliza tatizo hilo ambalo katika uongozi wa Ismail Aden Rage lilionekana kusumbua. Mara kadhaa lawama ziliibuka na yeye alikiri kwa kinywa chake kuwa kulikuwa na tatizo hilo.

Wachezaji waheshimiwe, wathaminiwe na kupata haki zao mapema. Hii itaongeza morali katika harakati za kuijenga Simba.

Sina tatizo na mipango yako Aveva, sera zako zilikuwa nzuri. Wanachama walikuamini na kukupa kura nyingi. Sasa muda wa utekelezaji uanzie hapa kwenye mazoezi.

Nimeambiwa utakiweka  kikosi kambini nchini Afrika kusini, tena kwa siku 17 kuanzia julai 20. Nadhani ni wazo zuri ambalo litawapa wachezaji utulivu mkubwa.

Kwa upande wa wanachama na mashabiki, kazi yenu ni moja tu. Ni kuunga mkono juhudi hizo na kusubiri ligi ianze ili muishangilie timu yenu. Mna haki ya kutoa maoni kwa viongozi wenu na benchi la ufundi, lakini sio lazima yachukuliwe. Ndio maana ya maoni.

Msiwape presha wachezaji na makocha wenu. Mkifanya mambo kwa utulivu na kumuacha kila mtu atekeleze majukumu yake basi itakuwa jambo jema.

Simba sc, kumekucha, agosti sio mbali. Ligi iko karibu. Sasa tulizeni akili katika maandalizi.

Kila la Kheri Mnyama Simba kuelekea msimu mpya. Tunasubiri kuwaona upya ili ladha ya utani wa jadi irudi kama zamani.



0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video