Wednesday, July 9, 2014

Kocha mkuu wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi (katikati) akiongea na Hassan Mwasapili (kushoto) na Richard Peter (Kulia)

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

0712461976


Imechapishwa Julai 2014, saa 5:37 asubuhi

DUNIA imepandwa na `mzuka bab kubwa` wa kutaka kujua nini timu nyingine ya Amerika (Argentina) itafanya katika mchezo wa leo wa nusu fainali ya pili ya kombe la dunia dhidi ya Uholanzi ya Van Gaal.

Argentina ikiwa na Lionel Messi inatarajiwa kufuta machozi ya Waamerika baada ya wenyeji Brazil kutandikwa kipigo cha kihistoria cha mabao 7-1 na Ujerumani.

Wakati kila mtu akiisubiri mechi hiyo kwa hamu, klabu ya Mbeya City fc iliyoleta ushindani mkubwa wa ligi kuu inatakiwa kufanya mambo muhimu kwa ajili ya kuendeleza mafanikio yake.

Msimu uliopita Mbeya city chini ya kocha bora wa Msimu, Juma Mwambusi ilishika nafasi ya tatu kwa kukusanya pointi 49 na kuiacha Simba katika nafasi ya nne.

Yanga walishika nafasi ya tatu na Azam fc walitwaa ndoo kwa mara ya kwanza katika historia yake.

Nafasi ya tatu kwa klabu changa kama Mbeya City yalikuwa mafanikio. Ugeni wa wachezaji katika michuano ya ligi kuu uliathiri kwa baadhi ya mechi kubwa kama ile dhidi ya Yanga, Simba na Azam fc.

Ligi kuu iligeuka kuwa maarufu zaidi kutokana na ujio wa Mbeya City fc.

Sasa timu hii inaelekea kucheza msimu wake wa pili. Miaka ya 80, Tukuyu Stars walipanda ligi kuu na kutwaa ubingwa, lakini msimu uliofuata walishuka daraja.

Baadhi ya watu wanadiriki kuwatabiria Mbeya City hali hii. Lakini ni mapema kusema yanaweza kutokea.

Mpaka sasa klabu hii inayomilikiwa na Halmashauri ya jiji haijaanza mazoezi rasmi. Kwa taarifa zilizopo ni kwamba wanatarajia kuanza maandalizi julai 15 mwaka huu.

Hawajafanya usajili mkubwa kwasababu sera yao haiwaelekezi kusajili wachezaji wengi wakongwe, wanajali soka lao la vijana. Wamemnasa mshambuliaji, Them Felix `Mnyama` kutoka kwa `wanankulukumbi ` Kagera Sugar.

Juma Mwambusi amebainisha kuwa kwasasa anaangalia uwezekano wa kusajili viungo wa ukabaji ili kuimarisha kikosi chake.

Mbeya City ni moja ya klabu niliyotarajia iingie kambini mapema kama walivyofanya Azam fc, na Ruvu Shooting.

Beki wa Mbeya City fc, Hassan Mwasapili akichuana na Erasto Nyoni wa Azam fc msimu uliopita katika dimba la Sokoine.

Kuchelewa kwa kambi kumechangiwa na majukumu ya kimataifa waliyokuwa nayo. Walienda nchini Sudan kushiriki michuano ya CECAFA Nile Basin Cup.

Hii ilikuwa changamoto nzuri kwao, na walitolewa hatua ya robo fainali. Waliporudi, waliamua kuwapa mapumziko wachezaji wao. Hawakuwa na jinsi na ndio maana mpaka sasa hawapo kambini.

Licha ya hayo, Mbeya City lazima watambue mambo kadhaa yaliyopo mbele yao yakiwemo yafuatayo:

Mosi; wana kibarua cha kuendeleza mafanikio ya msimu uliopita. Kuna haja ya kujipanga kwa hili. Moja ya tatizo la timu za Tanzania ni kushindwa kuendeleza pale walipofikia. Kwa mfano,  timu inachukua ubingwa, lakini msimu unaofuata inakuwa mbovu tena. Hili ni tatizo linalotokana na mipango mibovu ya viongozi pamoja na kutimua makocha. Leo hii Simba ya akina Okwi haipo tena. Walifanya mazuri, msimu uliofuata walipoteana.

Mbeya City fc wanatakiwa kujua hili, nafasi ya tatu yalikuwa mafaniko, lakini wanatakiwa kusonga mbele zaidi. Tunatarajia kuwoana wakiwa washindani wa ubingwa. Kwa bahati nzuri wamebakiza wachezaji wao wengi.

Mbeya City walishiriki michuano ya CECAFA Nile Basin nchini Sudan na kuishia hatua ya robo fainali

Ili kuendeleza mafaniko yao, lazima waje na mipango mingine. Kuna Dravko Logarusic wa Simba ambaye hatakubali kuona Simba inazingua tena. Kuna Marcio Maximo wa Yanga anayetaka kurejesha ubingwa na kuna Joseph Marius Omog wa Azam anayetaka kutetea ubingwa.

Mwambusi kazi haitakuwa rahisi kwake, lazima ajiandae mapema kwa ushindani wa msimu ujao. Nimewataja makocha watatu ambao ni `Levo` ya Mwambusi. Lakini wapo makocha wengine ambao watampa chanagamoto mfano, Fred Minziro wa JKT Ruvu, Tom Olaba wa Ruvu Shooting, Jackson Mayanga wa Kagera Sugar, Mecky Mexime wa Mtibwa Sugar  na wengineo.
Pili; Mbeya City itakuwa na wapinzani wengi kama ilivyo kwa Simba, Yanga na Azam fc.

Kila timu itakayokwenda Sokoine itakuwa inajipanga vilivyo. Upinzani utakuwa wa hali ya juu. Kutakuwa na uwezekano wa kukamia mechi kwasababu Mbeya City iko usawa wa kutafuta ubingwa. Pia mechi za ugenini zitakuwa na changamoto kubwa kama inavyotokea kwa Simba na Yanga.

Kagera Sugar ikicheza na Ruvu Shooting, kiwango huwa cha kawaida, lakini ikikutana na Yanga,  Simba, mpira unakuwa mgumu sana.

Kwahiyo tutegemee mechi ngumu zitazoikutanisha Mbeya City fc kwasababu ni timu tishio. Kwa mazingira haya, Juma Mwambusi ana kazi kubwa ya kuandaa kikosi chake.

Tatu; Baadhi ya wachezaji wa Mbeya City fc watakuwa wanakabwa kama akina Amisi Tambwe wa Simba sc, Mrisho Ngassa wa Yanga na Kipre Tchetche wa Azam.

Wachezaji wa timu ndogo huwa wanawakamia wachezaji hatari wa timu kubwa za Simba, Yanga na Azam fc. Msimu ujao, Mwegane Yeya, Paul Nonga, Saady Kipanga  watakuwa wanaangaliwa kwa jicho lingine. Lazima watakuwa wanawekewa ulinzi mkali. Pia kumbuka, Them Felix kaongezeka.

Kwa wachezaji hawa hatari wa Mbeya City, wanatakiwa kutambua hili na kuanza maandalizi ya mapema ili kutafuta mbinu mpya.

Nne: Mbeya City fc watambue kuwa watakosa huduma ya kocha msaidizi, Maka Andrew Mwalwisyi aliyemaliza mkataba wake na kuamua kuiacha klabu hiyo kwasababu anataka timu ya kuwa kocha mkuu. Hii imetokana na yeye kuwa na leseni B ya ukocha ya CAF.

Maka ni mwalimu mzuri na mwenye kipaji cha kuhamasisha na kushauri wachezaji. Anajua kufundisha soka la vijana na  anajua namna ya kuishi nao.

Hata wakati akiwa Mbeya City fc, mara kadhaa nilipata nafasi ya kukaa naye. Na kila tukiwa pamoja kambini, wachezaji walikuwa wanamtumia kwa mambo mengi ikiwemo kumuomba ushauri.

Kuondoka kwa kocha huyu, ni pigo. Najua wapo makocha wengi, lakini huwezi kufuta umuhimu wa Maka katika klabu ya Mbeya City fc.

Kinachotakiwa kwa viongozi wa klabu hii ni kutulia na kutafuta msaidizi wa aina ya Maka ili amsaidie Mwambusi.

Nguvu ya benchi la ufundi iongezwe. Mwambusi anatakiwa kupata mshauri na msaidizi wa aina ya Maka. Bila kufanya hivyo, kuna kitu kitapungua.

Tano; mashabiki wajipange mambo ya `Mtonyo`  mfukoni. Msimu uliopita, walisafiri kwa gharama zao kwenda kuishangilia timu kila ilipokuwa inakwenda kucheza mechi. Sasa isiwe nguvu ya soda, msimu ujao wanatakiwa kuendeleza moto ule ule.

Ina faida kubwa sana kwa wachezaji kila wanapoona kuna watu nyuma yao, hakika wanapata morali ya kuucheza mpira kwa ustadi.

Mashabiki wa Mbeya City msirudi nyuma. Kazeni buti mpaka kieleweke.


Mbeya City fc wadau wanatamani kuwaona katika kiwango kikubwa zaidi ya msimu ulipoita.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video