
Luiz Felipe Scolari, kocha wa Brazil
"Ni wakati
mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kazi yangu ya ukocha na siku mbaya zaidi
katika maisha yangu ya soka. Lakini maisha yanaendelea. Nani anawajibika kwa
matokeo haya? Ni mimi, ni mimi. Lawama za matokeo haya mabaya zinaweza kutuhusisha
wote, lakini mtu aliyeamua timu ya kucheza na mbinu nilikuwa mimi.
Lilikuwa chaguo langu. Tulijitahidi kufanya kila tuwezalo,
tulicheza kwa kiwango chetu cha mwisho-lakini tumeishia dhidi ya timu kubwa ya
Ujerumani. Hatukukata tamaa na kurudi nyuma. Tuliparaganyika na kupaniki baada
ya kufungwa bao la kwanza na kila kitu kiliharibikia hapo. Hata Ujerumani
hawawezi kuelezea ilitokeaje-lakini ni kwasababu ya ujuzi wao na unatakiwa kuheshimu
hilo.
Tunatakiwa kujiunza jinsi ya kukabiliana nalo. Ujumbe wangu
kwa watu wa Brazil ni huu. Tafadhali watusamehe kwa kiwango hiki. Ninaomba
radhi kwasababu hatujaweza kufika fainali-na tutajitahidi kushinda mechi ya nafasi
ya tatu. Bado tuna sababu ya kucheza.”

0 comments:
Post a Comment