
Imechapishwa Mei 23, 2014, saa 12:40 jioni
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Uongozi
wa Klabu ya Young Africans umeshangazwa na taarifa zilizoandikwa kwenye
mojawapo ya vyombo vya habari juu ya Wanachama wa Tawi la Tandale kusema
hawatambui kufutwa kwa Tawi lao ni za Ubabaishaji.
Mnamo
Mei 04, 2014 Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans Bw Yusuf Manji alitangaza
kulifuta Tawi la Tandale kutokana na kua chanzo cha migogoro ndani ya klabu kwa
kipindi cha mrefu, ili hali likiwa halina hadhi ya kuwa Tawi Kamili.
Kufutwa
kwa Tawi la Tandale kunatokana na kutotimiza idadi ya wanachama mia moja (100)
kama inavyojieleza kwenye Katiba ya Yanga SC, Ibara ya 6, kipengele cha 4
"Kutakuwa na uundaji wa matawi katika maeneo mbalimbali hapa nchini na nje
ya nchi. Kiwango cha chini ya idadi ya wanachama ambao wanaweza kunda tawi
kisipungue watu mia moja (100)".
Ibara
ya 13, kipengele cha 2 kinasema " Kutolipa ada zake za uanachama kwa muda
wa miezi sita mfululizo bila ya sababu maalum inayokubalika na Kamati ya
Utendaji"
Baadhi
ya Wanachama walijifuta uanchama wao kutokana na kushindwa kulipia ada zao za
uanachana kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita, kama inavyojieleza kwenye Katiba
kwamba mwanachama asipolipia ada yake zaidi ya miezi sita moja kwa moja
anajifuta uanachama wake.
Hivyo
Uongozi wa klabu ya Yanga SC unaomba Umma na Wanachama wake Duniani kote
watambue kuwa Tawi la Tandale lilifutwa kutokana na kutokidhi vigezo, huku
wanachama wake wengine watano wakijifuta uanachama kwa kushindwa kulipia ada
zao kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita.
Mwisho
wanachama wa klabu ya Yanga SC wanaombwa kulipia ada zao za uanchama mapema
kabla ya muda wao kumalizika ili waweze kushiriki mkutano mkuu wa marekebisho
ya Katiba utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi - Oysterbay Juni Mosi
2014.
Beno
Njovu
Katibu
Mkuu - Yanga SC
Mei
23, 2014
0 comments:
Post a Comment