
Mkono wa kwaheri: David Luiz amefuzu vipimo vya afya ili kukamilisha dili lake la paundi milioni 50 katika klabu ya PSG.
Imechapishwa Mei 23, 2014, saa 10:40 usiku
David Luiz
amafuzu vipimo vya afya na kukubaliana na vipengele binafsi vya mkataba
wake katika klabu ya Paris Saint-Germain utakaogharimu ada ya uhamisho
ya paundi milioni 50.
Nyota huyo mwenye miaka 27 atakuwa beki wa gharama zaidi duniani akivunja rekodi waliyoweka mabeki wawili wa PSG
Marquinhos na Thiago Silva.
Ofisa
wa PSG alikwea pipa leo hii kwenda kumfanyia vipimo vya afya beki huyo
katika kambi ya timu ya Taifa ya Brazil leo ijumaa.

Shukurani kwa Muumba:Nyota wa Chelsea , Luiz alicheza mechi yake ya mwisho na ataigharimu PSG paundi milioni 50

Ulimi nje nje: Luiz akishangilia ubingwa wa ligi ya Europa mwaka 2013 baada ya kuifunga Benfica mechi ya fainali.
0 comments:
Post a Comment