Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 23, 2014 saa 12:30 jioni
Tanzania inaendelea kufanya vizuri kwenye Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) kwa upande wa mpira wa miguu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 baada ya leo (Mei 23 mwaka huu) baada ya kuwachapa wenyeji Botswana mabao 2-0.
Mabao
ya Tanzania katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa SSKB jijini Gaborone
yalifungwa na David Uromi dakika ya sita huku Anthony Amede akitupia la pili
dakika ya 46.
Katika
mechi yake ya kwanza, Tanzania ilitoka sare ya bao 1-1 na Mali ambapo michezo
hiyo inaoneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha SuperSport cha
Afrika Kusini.
Tanzania
itacheza mechi yake ya tatu keshokutwa (Mei 25 mwaka huu) dhidi ya Swaziland,
itakuwa tena uwanjani Mei 27 mwaka huu kuikabili Nigeria wakati mechi ya mwisho
itafanyika Mei 29 mwaka huu dhidi ya Afrika Kusini.
0 comments:
Post a Comment