
NAHODHA
wa zamani wa Uholanzi katika fainali za kombe la dunia, Ruud Krol amefukuzwa
kazi ya ukocha mkuu katika klabu ya Tunisia ya Esperance ikiwa ni wiki kadhaa
zimepita tangu awaongoze kutwaa ubingwa wa ligi kuu katika nchi hiyo ya
kaskazini mwa Afrika.
Krol
amefukuzwa kazi saa kadhaa baada ya timu yake kufungwa mara ya pili mfululizo
katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika mwishoni mwa wiki, na taarifa
ya klabu imesema Mfaransa Sebastien Desabre atatangazwa kuwa mrithi wake.
Kocha
huyo mwenye miaka 65 amekuwa kocha wa kwanza nchini Tunisia kushinda mataji ya mawili
akiwa na klabu mbili tofauti baada ya
kuwapa ubingwa Esperance dhidi ya timu yake ya zamani ya SC Sfaxien mapema
mwezi huu.
Krol
aliachana na SC Sfaxien mwezi novemba mwaka jana baada ya kuwaongoza kutwaa
ubingwa wa ligi kuu ya Tunisia na kombe la shirikisho.
Mwezi
Oktoba na Novemba mwaka jana, Mholanzi huyo pia aliiongoza kwa muda timu ya
taifa ya Tunisia dhidi ya Cameroon katika mchezo wa kufuzu fainali za kombe la
dunia. Cameroon ilishinda kwa wastani wa mabao 4-1.
0 comments:
Post a Comment