Imechapishwa Mei 26, 2014, saa 12: 21 jioni
BRENDAN Rodgers amepewa ofa nzuri ya
kazi katika klabu ya Liverpool kwa kusaini mkataba mwingine utakaomfanya
akae muda mrefu zaidi Anfield.
Rodgers,
aliyebakiwa na miezi 12 katika klabu hiyo amepewa zawadi hiyo ya
mkataba baada ya kufanya vizuri ligi kuu na sasa amemwaga wino katika
mkataba mpya unaosemekana kumuweka
Merseyside mpaka 2018.
Liverpool
walimaliza pointi mbili tu nyuma ya mabingwa Man City tangu mwaka 1990
na walionesha kiwango kikubwa mno chini ya Rodgers na kuwavutia Wamiliki
wa klabu hiyo, raia wa Marekani.
Tangu
Rodgers ajiunge na Liverpool 2012 akitokea Swansea City amekuwa kivutio
kwa mashabiki na wamiliki wa klabu hiyo na sasa wanajiandaa kumpa dau
la kutosha kufanya usajili kwa ajili ya msimu ujao na michuano ya UEFA.
Rekodi za Rodgers katika klabu ya LIVERPOOL
Ameongoza mechi 97, ameshinda mechi 54, sare 21 na kupoteza mechi 22 .
Amefunga magoli 206 na kufungwa magoli 118 na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni (+88)
Asilimia ya ushindi ni 55.67
Amefunga magoli 206 na kufungwa magoli 118 na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni (+88)
Asilimia ya ushindi ni 55.67
Mmiliki John Henry na mwenyekiti wa klabu Tom Werner kwa pamoja wamesema:
"Tuna bahati ya kuongozwa na mtu mwenye kipaji kikubwa katika klabu yetu na tumeweza kuonesha kiwango cha juu na katika yeye tumejenga imani yetu na tutafanikiwa maono yetu".
"Brendan yuko katika mioyo yetu, kama wamiliki, tunajitahidi kufanikiwa uwanjani. Msimu huu umempa imani kila mmoja kuwa tunaweza kuleta mafanikio Liverpool na tunajitahidi kufanya kazi pamoja ili kufanikisha hilo".
"Wachezaji na mashabiki wameweka wazi jinsi ambavyo Brendan ni muhimu katika mafanikio yetu, hivyo tumeamua kumwamini zaidi na kumpata mkataba mrefu zaidi ambao utamfurahisha kila mmoja wetu".
0 comments:
Post a Comment