
NA DAVID NGALEMA
Imechapishwa Mei 23, 2014, saa 11:15 jioni
Siku chache zilizopita, Ryan Giggs alitangaza kustaafu soka. Atajiunga Luis Van Gaal kwenye benchi la ufundi la Man United kama kocha msaidizi.
Ni huzuni kubwa kutomuona tena dimbani akiwa na
jezi yake namba 11, badala yake tutaendelea kumuona akiwa benchi na Luis Van
Gaal . Sidhani kama ni sahihi kumpa mtu mwingine namba (11) ya Giggs aitumie ,
Sio kwa heshima tu, bali ni kwa mambo makubwa aliyoyafanya huyu jamaa akiwa Man
United
Giggs ana historia ya kipekee katika ulimwengu wa
soka, Ni mchezaji pekee aliyefunga goli kwenye kila msimu wa ligi kuu tangu aanze
kucheza kwenye msimu wa 1990-91 mpaka 2013-14. Alifunga goli lake la kwanza
kwenye Manchester Derby (nikimaanisha dhidi ya Man City), Manchester United
ikishinda 1-0. Ikumbukwe kuwa alipitia Man City kabla ya kujiunga na Mashetani
wekundu mwaka 1987.
Giggs ni mchezaji wa kwanza kushinda mfululizo
tuzo ya Young player of the year mwaka 1992 na 1993, Wayne Rooney ni moja kati
ya wachezaji waliowahi kushinda mara mbili mfululizo tuzo iyo.
Giggs katika historia yake aliweza kufunga magoli
kadhaa ya kusisimua sana yakawa ni kati ya magoli bora ya msimu, lakini goli
ambalo halitosahaulika milele ni lile alilowafunga Arsenal kwenye nusu fainali
ya FA, akichukua mpira uliopotezwa na kiungo Patrick Viera kutoka katikati ya
uwanja akipiga chenga kwa spidi na kwa kujiamini akikatiza katika ngome imara
iliyoundwa na beki kama Tony Adams, Martin Keown na Lee Dixon na kuweka mpira
nyavuni akimuacha David Seaman hana la kufanya langoni.
Akiwa Manchester United ameweza kushinda mataji
makubwa mbalimbali kama UEFA champions league, EPL, FA. Msimu wake wa mwisho
2013-14 alikabidhiwa kuiongoza Man United katika mechi 4 zilizobakia baada
kutimuliwa David Moyes. Kitendo cha Giggs kuaminika na kupewa nafasi hiyo,
kinaonyesha yeye ni mtu wa aina gani. Ni ngumu kupata mtu kama Giggs tena
kwenye ulimwengu wa soka.
Kuna tetesi kwamba kijana Adnan Januzaj anaweza
kupewa jezi namba 11 ya gwiji Ryan Giggs. Sidhani kama huyo kinda anaweza kuvaa
viatu vilivyoachwa na Giggs, Ni vikubwa mno. Januzaj anaweza kuwa ni mchezaji
mzuri, lakini kila nikimuona uwanjani na namba 11, nitakua namkumbuka Ryan
Giggs.
Ningependa
Januzaj asihusishwe na hii namba, inaweza kumuharibia mpira wake huyu bwana
mdogo. Acha Januzaj awe Januzaj, aendelee kuvaa namba yake 44 au wampe namba
nyingine lakini sio 11.
Ikiwa WestHam na Ac Milan waliweza kufuta jezi
namba sita kwa kuwaenzi Bobby Moore na
Franco Baresi, Kwanini Man U wasifanye hivyo?
Hata Bongo, usitegemee kuona jezi namba 30
ikitumika tena Msimbazi, Hii ni kutokana maamuzi ya kuifuta ili kumuenzi
marehemu Mafisango.
Mimi huwa namuita Sir Ryan Giggs, mwenye namba 11
mgongoni ya maajabu.
Imeandikwa na David Ngemela @muggypro. Mwanafuzi
wa Chuo kikuu cha habari.
0 comments:
Post a Comment