
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 30, 2014, saa 1:55 usiku
TIMU ya Taifa ya Kenya, `Harambee stars` imelazimisha sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Comoros katika mchezo wa marudiano wa kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika, AFCON mwakani nchini Morocco.
Harambee Stars waliibuka na ushindi wa bao 1-0
katika mchezo wa kwanza mjini Nairobi na sare ya leo inawafanya wasonge mbele
kwa wastani wa mabao 2-1.
Hata hivyo katika mchezo wa leo, Kenya ilimkosa
mchezaji wake wa kimataifa, Denis Oliech ambaye aliondolewa kikosini kwa madai
ya utovu wa nidhamu.
Rais wa shirikisho la soka Kenya,
KFF, Sam Nyamweya amesema wamepambana kwa nguvu zote kuhakikisa kuwa wanapata
matokeo.
Nyamweya aliongeza kuwa Comoros
walijidhatiti katika mchezo wa leo, lakini wanashukuru vijana wao wamejituma na
kusonga mbele.
Kuelekea katika mchezo wa Taifa
Stars dhidi ya Zimbabwe keshokutwa jumapili, Nyamweya ameitakia kila la heri
timu ya taifa ya Tanzania.
Rais huyo alisema Tanzania ni
majirani wazuri wa Kenya, hivyo watafurahi kuona Taifa stars inasonga mbele
kama wao.
Mechi nyingine inayopigwa leo ni
baina ya Sudan Kusini dhidi ya Msumbiji.
Mechi ya kwanza iliyopigwa mjini
Maputo, Msumbiji waliibuka na ushindi wa mabao matano.
Msumbiji wanahitaji kutofungwa
mabao zaidi ya matano ili kusonga mbele, na wakishinda watakutana na mshindi wa
jumla baina ya Taifa Stars dhidi ya Zimbabwe.
0 comments:
Post a Comment