

Kipa akihangaika kuokoa shuti la Sturridge bila mafanikio


Imechapishwa Mei 31, 2014, saa 1:00 asubuhi
ENGLAND
ilifanya kazi kubwa ya kuvunja ngome imara ya timu ya taifa ya Peru na
kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mechi ya kimataifa ya
kirafiki kujiandaa na kombe la dunia kwenye uwanja wa Wembley mjini London.
England
wanaotarajia kuweka kambi yao ya mwisho Miami walipata nguvu kwa bao la kwanza
la Daniel Sturridge katika dakika ya 32 na kudumu kipindi kizima cha kwanza.
Mabao
mawili ya kipindi cha pili kupitia kwa beki wa kati Gary Cahil na Phil Jagielka yaliweza kuwapa ushinidi wa
kwanza baina ya mataifa haya tangu walipokutana miaka 52 iliyopita ambapo
ilikuwa ni katika kombe la dunia mwaka 1962 nchini Chile.
Peru
walioshindwa kufuzu fainali za kombe la dunia nchini Brazil kutokana na kufanya
vibaya katika kampeni za kufuzu katika bara la Marekani kusini, walikuwa na
ngome imara ya ulinzi na Jean Deza alisimama vizuri sehemu ya kiungo, huku
golikipa wa England Joe Hart akiokoa michumo miwili.
“Ilikuwa
ni sherere nzuri ya kutuaga kuelekea kombe la dunia kwa mashabiki wengi
kufurika uwanjani”. Alisema kocha wa England, Roy Hodgson wakati akizungumza na
ITV.
“Tulitakiwa
kuwa wavumilivu kwasababu tulitawala vipindi vyote. Ilikuwa kipimo kizuri
wakati huu wiki mbili zikisalia. Nimefurahi kuona mashabiki elfu 85 wamekuja
kututakia kila la kheri”.
“Ushindi
wa mabao 3-0 ni mafanikio mazuri. Pia ilikuwa kipimo kizuri kwa wachezaji
vijana wakati huu wakiaga Wembley”.
Kikosi
cha England kilikuwa: Hart, Johnson, Cahill, Jagielka
(Smalling 73), Baines (Stones 75), Gerrard (Wilshere 64), Henderson, Lallana
(Milner 73), Rooney (Sterling 66), Welbeck, Sturridge (Barkley 82). Subs not
used: Foster, Lampard, Lambert, Flanagan, Forster.
Goals:
Sturridge 32, Cahill 65, Jagielka 70.
0 comments:
Post a Comment