Na Mwandishi Wetu, Tanga
Imechapishwa Mei 30, 2014, saa 7:10 jioni
MCHAKATO wa usajili wa Klabu ya Coastal Union
umeanza hivi karibuni kwa ajili ya maandalizi ya Ligi kuu msimu ujao ambao
utaanza Mwezi Agosti mwaka huu lengo likiwa kuhakikisha wanarudisha heshima yao
kwa kuchukua kombe hilo.
Katika kuthibtisha hilo litawezekana tayari uongozi wa klabu hiyo umeanza kuwasainisha mikataba baadhi ya wachezaji wapya na wazamani waliokuwepo kwenye timu hiyo ambapo hafla hiyo ilifanyika kwenye makao makuu ya klabu hiyo.
Akizungumza makao makuu ya klabu hiyo,Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi amesema Wachezaji wapya waliosajiliwa na kushuhudiwa wakisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo kuwa ni mchezaji kutoka nchini Nigeria Ike Bright Obina ambaye alisaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo.
Mchezaji huyo msimu uliopita alikuwa akiichezea Ashanti United kwa mkopo kwa kipindi cha miezi sita akitokea Klabu ya Azam FC ambapo baada ya kusaini mkataba huo ataichezea timu hiyo yenye makazi yake katikati ya jiji la Tanga.
Mchezaji mwengine mpya aliyesaini mkataba huo ni mshambuliaji wa Ashanti United Hussein Sued wakati mchezaji wa zamani aliyesaini
mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo ni Razack Khalfani baada ya ule wa awali kumalizika.
Katibu huyo alimtaja mchezaji mwengine kuwa ni aliyekuwa Beki wa timu ya Mgambo Shooting,Bakari Mtama lengo likiwa kupata saini ya mchezaji huyo ambaye alionekana kuwa tishio msimu uliopita.
Amesema wachezaji wote hao ni mapendekezo ya Kocha Mkuu wa timu hiyo,Yusuph Chippo aliyeyakabidhi kwa uongozi wao ili waweze
kuyafanyika kazi kwa ajili ya kuimarisha timu hiyo kabla ya kuanza msimu mpya.

Kwa upande wake,Ofisa Habari wa timu hiyo,Oscar
Assenga amesema malengo makubwa ya timu hiyo kuhakikisha wanafanya vizuri msimu
ujao ili waweze kushiriki makubwa ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
0 comments:
Post a Comment