Wednesday, April 16, 2014



LIGI kuu nchini Uturuki haina jina kubwa ukilinganisha na ligi zenye mvuto mkubwa barani ulaya kama vile England, Hispania, Ujerumani na Italia.
Kutokana na hali hiyo, kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa Uturuki, klabu ya Galatasaray, Mholanzi Wesley Sneijder ameanza kuonekana wa kawaida sana na kuwa hatarini kulikosa kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Sneijder alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Uholanzi, lakini mambo yamebadilika baada ya kwenda Uturuki na sasa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Uholanzi, Louis Van Gaal amekaririwa akisema kuwa nyota huyo yawezekana asijumuishwe katika kikosi chake.
Baada ya maneno ya kocha Gaal, wachezaji wenzake wanasemaje juu ya maamuzi ya kumuacha Sneijder?
Winga machachari wa klabu ya Bayern Munich na timu ya Taifa ya Uholanzi, Arjen Robben amemkazia bosi wake na kusema
Sneijder bado ni mtu muhimu katika kikosi chao  na anaweza kuisaidia nchini yake.
“Wesley ni mchezaji muhimu. Nilishaongea hili toka mwanzo na sio siri kuwa namkubali sana jamaa”.
“Anapocheza katika kiwango chake ambacho anacheza sasa, Wesley ni mchezaji anayeongeza kitu cha ziada katika timu. Unahitaji mchezaji kama yeye kombe la dunia”.
“Nampenda sana Wesley. Kiukweli hatuwezi kufananisha kiwango chake cha miaka minne iliyopita. Umri unakwenda na mambo yanabadilika. Lakini bado anaongeza kitu Fulani kwa timu yetu”. Amesema Robben.
Sneijder ameichezea mechi 97 timu ya Taifa ya Uholanzi na kufunga mabao 26.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video