Wednesday, November 6, 2013


Wamanchi wa vijini vya Itongo itale na  Mwanhili Wilayani Kishapu, Mkoani Shinyanga, waliokumbwa na maguriko na kupoteza nyumba, vyakula na mifugo, wakimsikiwa mkoa wa  huo Ally Rufunga alipowatembelea na kutoa adahi ya sh16.6 za kuwasaidia. Picha na Suzzy Butondo
Na GLADNESS MUSHI, MERU
CHAMA cha Mapinduzi Wilaya ya Meru Mkoa wa Arusha kimeweka utaratibu maalumu wa kuhakikisha kuwa kinashirikiana na taasisi mbalimbali za fedha ili kuweza kutoa elimu pamoja na huduma mbalimbali za kifedha hasa maeneo ya vijijini huku lengo likiwa ni kuongeza ufanisi wa kiuchumi
Hayo yamelezwa jana na Mwenyekiti wa Chama hichoBw Furaini Mungure wakati akiongea na wananchi wa Mareu kuhusiana na umuhimu wa kujiunga na taasisi za fedha
Mungure alisema kuwa mpango huo utaanza hivi karibuni na utafadhiliwa na chama hicho ambapo taasisi hizo zitaitwa na kisha kuanza kutoa elimu juu ya masulaa mbalimbali ya kifedha
Alifafanua kuwa mpango huo utaenda katika maeneo ya vijijini zaidi ambapo mpaka sasa takwimu zinaonesha kuwa pamoja na kuwepo kwa huduma nyingi za kifedha katika maeneo ya mijini lakini vijijini bado wananchi wengi hawajui hata umuhimu wa kutumia huduma hizo
“tunatazamia kuona kuwa sio kwamba tunaambatana na siasa pekee bali tuwasaidie hawa wananchi wa vijijini katika wilaya hii ya Meru wawe na uwezo wa kujua na kutambua umuhimu wa huduma za kifedha kwani hii kama itafanikiwa basi itachangia sana kuongeza hata uchumi wa Meru”aliongeza Mungure
Mbali na hayo alidai kuwa kwa sasa kuna umuhimu mkubwa sana wa Mabenki nayo kujiwekea utaratibu wa kutoa elimu ya masuala mbalimbali kama vile ukopaji hasa vijijini kwani wengi sana wanaokopa huishia kwenye mashindano ya nguo lakini hata Vinywaji
Alisema,kama wananchi watapata elimu ya kutosha hususani kwenye suala zima la ukopaji ni wazi kuwa mikopo inayotolewa katika maeneo ya vijiji itaweza kusababisha mabadiliko ya uchumi lakini pia hata idadi ya wakopaji nayo itaongezeka sana.
“Hizi benki zisikubali kutoa mikopo na kudai marejesho lakini ziwe na mrejesho mzuri ambao utasaida hata wasiokopa kuona kuna umuhimu wa kukopa kwa mfano hapa Meru vijiji vyetu vina uwezo mkubwa sana wa kuimarisha uchumi kutokana na mikopo lakini mara nyingine wanakosa fursa hivyo kuna umuhimu wa kubadilika kuanzia sasa’aliongeza Mungure

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video