Naibu
Mkuu na Mshauri wa Masuala ya Kisiasa wa Ubalozi wa China nchini
Tanzania, Li Xuhang akizungumza na raia wa China wanaoishi Tanzania na
wananchama wa Chama cha Wachina Tanzania juu ya kufuata sheria za
Tanzania na China.

Lin
Zhiyong Mkuu wa Wakikilishi wa Masuala ya Kiuchui na Kibiashara katika
ubalozi wa China nchini Tanzania akizungumza na raia wa nchi yake
wanaoishi Tanzania.

Naibu
Mkuu na Mshauri wa Masuala ya Kisiasa wa Ubalozi wa China nchini
Tanzania, Li Xuhang (kulia) akizungumza na raia wa China wanaoishi
Tanzania.

Baadhi
ya raia wa China wanaoishi Tanzania wakiwasikiliza viongozi wa ubalozi
wa nchini hiyo (hawapo pichani) baada ya wenzao kukamatwa na Jeshi la
Polisi nchini kwa tuhuma za kufanya magendo ya meno ya tembo.
Hussein Makame, MAELEZO
CHINA
ina shirikiana na Tanzania kufanya uchunguzi wa tuhumu zanazowakabili
raia watatu wa nchi hiyo wanaodaiwa kukamatwa wakiwa na meno ya tembo
706 jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Hayo
yamesemwa na Naibu Mkuu na Mshauri wa Masuala ya Kisiasa wa Ubalozi wa
China nchini Tanzania, Li Xuhang wakati alipozungumza na wanahabari
kwenye ubalozi wa nchi hiyo kwenye mkutano wa Chama cha Wachina Tanzania
uliofanyika kwenye ubalozi wa nchi hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Alisema
kuwa Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing pamoja na ubalozi wake
wanalaani vikali kitendo hicho cha mauaji ya tembo na magendo ya meno
yake na kwamba nchi hiyo iko tayari kushiurikiana na Tanzania kupambana
na wahalifu.
Aliongeza
kuwa Serikali ya China inaiunga mkono kwa dhati Serikali ya Tanzania
kipingana na magendo ya meno ya tembo na Jeshi la Polisi lake linapenda
kushirikiana na Jeshi la Polisi la Tanzania kupambana na wahalifu.
Alifafanua
kuwa ubalozi huo umestushwa na habari hiyo iliyoripotiwa na baadhi ya
vyombo vya habari nchini na kwamba sasa upande wa China unafanya
uchunguzi kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania ili kupata uhalisia
wa habari hiyo.
“Jana
na leo tumepeleka Maafia wa Ubalozi wetu kuchunguza kwanza kuthibtisha
utambulisho na pia tumeliambia Jeshi la Polisi kwamba hawa watu watatu
kkama ni raia wa China haki zao za msingi lazima zilindwe”, alisema
Xuhang.
Aliongeza
kuwa “Tumeamua kufanya uchunguzi wa kina kwa sababu hatuwezi kufanyia
kazi taarifa za vyombo vya habari, hivyo lazima tuthibitishe taarifa
hizi na ikiwa ni za kweli tutakuwa tayari kuisaidia Serikali ya Tanzania
kuwafikisha mahakmani wahusika”
Alifafanua
kuwa kufanya magendo ya meno ya tembo ni kosa kubwa la jinai kwa nchi
ya China na adhabu kali inatolewa kwa mtu anayepatikana na kosa hilo
ikiwemo itakutwa na kilo sita za meno hayo anafungwa jela miaka kumi au
zaidi.
“Ikiwa
utapatikana na hatia ya meno ya tembo ya zaidi ya kilo sita unaweza
kuhukumiwa jela miaka zaidi ya kumi au kunyongwa kabisa, kwa hiyo
Serikali ya China inaongoza duniani kwa kutoa adhabu kali kwa kosa hilo”
alisema Xuhang.
Aliwataka
raia wote wa China wanaoishi Tanzania kufuata Sheria za China na za
Tanzania na kwamba wasifanye kitendo chochoe kinachokwenda kinyume na
sheria kama vile kufanyamagendo ya meno ya tembo.
0 comments:
Post a Comment