Rais Jakaya Mrisho Kikwete  wakati
 alipokutana na Waziri wa Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la 
Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath Pushpakumara (shati jeupe)  na 
ujumbe wake mjini Colombo, Sri Lanka, kuzungumzia njia za kushirikiana kukabiliana na maradhi ya mazao likiwamo zao la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko.  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi inayotokana na zao la mnazi toka kwa Waziri
 wa Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, 
Mheshimiwa Jagath Pushpakumara (shati jeupe)  na ujumbe wake mjini 
Colombo, Sri Lanka, kuzungumzia njia za kushirikiana kukabiliana na maradhi ya mazao likiwamo zao la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi inayotokana na zao la mnazi toka kwa Waziri

Picha
 ya pamoja ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete  wakati na Waziri wa Maendeleo
 ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa 
Jagath Pushpakumara (shati jeupe)  na ujumbe wake mjini Colombo, Sri 
Lanka, kuzungumzia njia za kushirikiana
kukabiliana na maradhi ya mazao likiwamo zao la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko.
PICHA NA IKULU
 ———————————————————–
Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete 
amesema kuwa Serikali  imedhamiria kukabiliana na maradhi ya mazao 
likiwamo zao la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko.
Aidha,
 Rais Kikwete amesema kuwa ni muhimu kwa Serikali kuchukua hatua za 
kukabiliana na tatizo la minazi kwa sababu watu wengi katika baadhi ya 
maeneo ambayo uchumi wake unategemea zao la mnazi wanakabiliwa na hatari
 ya kweli kweli ya kuathirika kwa maisha yao.
Rais
 Kikwete ametoa uhakikisho huo jana, Jumamosi, Novemba 16, 2013, wakati 
alipokutana na Waziri wa Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la 
Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath Pushpakumara na ujumbe wake 
mjini Colombo. Waziri huyo aliandamana na Mwenyekiti wa Taasisi ya 
Utafiti ya Minazi ya Sri Lanka.
Rais
 Kikwete yuko nchini Sri Lanka kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi 
Wanachama wa Jumuia ya Madola (CHOGM) unaomalizika leo, Jumapili, 
Novemba 17, 2013. Mkutano huo wa siku tatu, ulianza juzi, Ijumaa, 
Novemba 15, 2013.
Mheshimiwa
 Pushpakumara na ujumbe wake walikuwa wanamwelezea na kumkabidhi Rais 
Kikwete Ripoti ya Magonjwa ya Minazi iliyoandaliwa na wataalam wa minazi
 wa Sri Lanka ambao walitembelea Tanzania Julai mwaka huu.
Wataalam
 hao walitembea Tanzania na kufanya utafiti kuhusu ugonjwa unaolikabili 
zao la minazi kufuatia ahadi ya Rais Mahinda Rajapaksa aliyoitoa kwa 
Rais Kikwete wakati alipofanya ziara rasmi ya Tanzania Juni 27, 2013, na
 baadaye kushiriki katika Mkutano wa Smart Partnership Juni mwaka huu. 
Rais
 Rajapaksa alitoa ahadi hiyo baada ya kuelezwa na Rais Kikwete kuhusu 
zao la kukauka kwa minazi nchini. Mnazi ni zao muhimu sana katika uchumi
 wa Sri Lanka na ni zao tegemeo kwa wananchi wa Taifa-Kisiwa hilo 
kilichoko kusini mashariki mwa India katika Barahri ya Hindi.
Wataalamu
 waliofuatana na Waziri huyo wamemwambia Rais Kikwete kuwa ugonjwa 
unaolikabili zao hilo la minazi ambao pia unashambulia minazi katika 
eneo la Caribbean hauna tiba kwa sababu mpaka sasa hakuna taasisi yoyote
 ya utafiti imegundua dawa hiyo.
Wataalam
 hao ambao walikaa Tanzania kwa wiki moja, zikiwamo siku mbili katika 
Zanzibar, wanasema kuwa zao hilo la mnazi, kama ilivyo katika nchi 
nyingine zinazolima zao hilo, lina uwezo mkubwa wa kusaidia uchumi 
kupitia viwanda vidogo vidogo.
Wakati
 wakiwa Tanzania, wataalam hao wa Sri Lanka walifanya uchunguzi na 
utafiti kwa karibu na wataalam wa Taasisi ya Utafiti ya Kilimo ya 
Mikocheni (MARI).

0 comments:
Post a Comment