Mshambuliaji
wa Kagera Sugar mwenye magoli 7 kwa sasa, Themi Felix (anayekimbia
pichani) amesema washambuliaji wanaoongoza kwa mabao kwa sasa ni hatari
………………………………………………………………………..
Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
MSHAMBULIAJI
hatari wa Kagera Sugar, Themi Felix mwenye magoli 7 kwa sasa
amewakubali washambuliaji wenzake wa ligi hiyo kuwa wako vizuri sana na
wanastahili pongezi kwa uwezo wao mkubwa.
Akizungumza na mtandao wa MATUKIO DUNIANI,
Felix ambaye alikuwa anawania tuzo ya mwanaspoti bora wa mwaka
inayoandaliwa na gazeti la michezo la Mwanaspoti amekiri kuwa
waliomtangulia katika mabao wanaiweza kazi na yeye anapata changamoto
kubwa zaidi.
“Kuna
washambuliaji kama Amisi Tambwe wa Simba, Khamis Kiiza wa Yanga, Juma
Luizio wa Mtibwa Sugar, hakika wanaweza kazi na wanaonesha uwezo wa
hali ya juu kufumania nyavu, lakini na mimi najipanga vizuri zaidi ili
kuendelea kupambana nao”. Alisema Felix.
Ferlix
aliongeza kuwa ligi ya mwaka huu imekuwa ngumu sana na ukizingatia
imekuwa na vijana wengi wenye uchu wa kupata mafanikio.
Pia
alisema kuwa timu ndogo kama Mbeya City zimebadili sura na mtazamo wa
ligi yetu, ingawa wasiwasi wake ni kuwa mzunguko wa pili hana uhakika
kama watahimili mikikimikiki ya vigogo Simba na Yanga.
“Kwa
ligi yetu na utamaduni wa timu zetu, sina imani kama Mbeya City
wataendelea kuwepo kule juu, lakini nisiseme sana kwani unaweza kusema
hawatakuwepo kumbe wakawepo, tusubiri kuona itakuwaje”. Alisema Felix.
Felix
alisema kwa sasa wamevunja kambi, lakini yeye akiwa mchezaji anaendelea
na mazoezi ya kujiweka sawa kwani akikaa tu atajikuta anaanza upya.

0 comments:
Post a Comment