Monday, November 11, 2013

1 
Beki wa Kushoto wa Maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa, Ruvu Shooting Stars, Stephano Mwasyika (Kulia) akiwa kwenye shughuli yake wakati walipokutana na Mnyama Simba SC mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania bara mwaka huu
…………………………………………………………………………………………………………………………………
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Beki wa kushoto wa maafande wa Ruvu Shootinga ambaye pia aliwahi kuzichezea klabu za Prisons, Moro United, na Mabingwa Yanga msimu uliopita, Stephano Mwasyika amewashauri waamuzi wa ligi kuu soka Tanzania bara kujenga utamaduni wa kuthamini mawazo ya wachezaji wanapochezesha mechi mbalimbali.

Mwasyika amesema waamuzi wengi wa kitanzania hawana uwezo wa kuwasikiliza wachezaji uwanjani hata kama wamekosea kutafsiri sheria.

“Mwamuzi anaweza kukosea kitu fulani, mchezaji unamfuata, hataki kukusikiliza. Soka sio uhasama jamani, sijui hawajifunzi kwa wenzao wa Ulaya, mara zote wamekuwa wakizungumza na wachezaji kuhusu mambo mbalimbali ya uwanjani, hasa wanapokosea”. Alisema Mwasyika.

Beki huyo anayesifika kwa kupiga pasi za uhakika aliongeza kuwa waamuzi ndio wenye maamuzi ya juu katika mechi, lakini lazima wakubali kuwa wao ni binadamu, hivyo kukosea ni kawaida.
“Katika kila kazi, kukosea kupo tu, hakuna ambaye hakosei. Lakini ukikosea na ukakubali kuwa umekosea, inakuwa nzuri zaidi. Waamuzi lazima wajifunze.”. Alisema Mwasyika.

Mwasyika alisisitiza kuwa baadhi ya waamuzi kwa kukosa ustaarabu wanadiriki mpaka kutoa matusi ya nguoni.

“Mimi siwezi kutaja mtu, lakini kwenye mechi moja pale uwanja wa Taifa msimu huu, kuna mwamuzi mmoja alimtukana mchezaji matusi ambayo siwezi kuyasema. Nawaomba wajifunze kutoka `Videoni` namna ya kuwasiliana na wachezaji, na ndio maana kunatokea mambo ya kukunjana na kupigana”. Alisema Mwasyika.

Hata hivyo, Mwasyika amewapongeza waamuzi waliochezesha ligi kuu mzunguko wa kwanza kwa madai kuwa wamejitahidi kufanya kazi yao, lakini wakijifunza suala la mawasiliano na wachezaji, itawajengea ufanisi katika kazi yao.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video