Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha wa washika bunduki wa London Kaskazini, nchini England, klabu ya Arsenal, Mfaransa mzee Arsene Wenger amepewa ruksa na uongozi wa klabu yake kuhusu kuamua usajili wa mashambuliaji hatari wa Liverpool, raia wa Uruguay, Luis Suarez kwa ofa ya pauni milioni 40.
Nyota huyo ni chaguo namba moja la Arsenal katika dirisha hili la majira ya kiangazi la usajili barani Ulaya, na tayari walishatuma ofa ya pauni milioni 30, lakini Liverpool walitupilia mbali.
Mtandao wa FULLSHANGWE kupitia mtandao rafiki wa Sporstmail ulishaweka wazi wiki hii kuwa The Gunners waliongeza mzigo hadi kufikia pauni milioni 35, lakini bado waligonga mwamba kwani majogoo hao wa jiji walishaweka wazi kuwa wao wanahitaji dau la pauni milioni 40
Ofa ya pauni miloni 40 ni rahisi kwa Suarez kuondoka Anfield, na kwa vile Asernal wamemruhusu Wenger kutoa dau hilo, basi ana dakili zote za kumnasa.
 Wakala wa Suarez bwana Pere Guardiola, aliweka wazi kuwa mtu mwenye ofa hiyo akaye naye wazungumze , wakati huo huo Liverpool walikubali kumuachia nyota  huyo endapo timu yoyote itatoa dau hilo.
Mbali na Suarez, Wenger pia alikuwa na nia ya kuwasajili,  Gonzalo Higuain na  Wayne Rooney, lakini ngoma imekuwa nzito sana.
Pesa kubwa: Arsene Wenger amepewa ruksa ya kutumia pauni milioni 40 kumsajili Luis Suarez
Dili la nguvu: Wakala wa Suarez alisema kama Arsenal watafikisha dau linalotakiwa, basi Liverpool watashawishika kusikiliza ofa
Karudi kibaruani: Brendan Rodgers na kikosi cha Liverpool wamerudi mazoezini kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England.
Kocha wa Liverpool,  Brendan Rodgers anaamni Suarez atajiunga na kikosi chake na ataendelea kucheza katika dimba la Anfield
Suarez yupo katika rada za Asernal na yeye alishatangaza kutaka kuihama klabu yake ya sasa
 Arsene Wenger alipigwa picha hii wakati akiwa na klabu yake katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu
Wasiwasi: Dili la Higuain litakuwa limeshakufa baada ya Wenger kuelekeza nguvu zote kwa SuarezWakati huo huo beki wa Arsenal, Bacary Sagna amesisistiza kuwa hataondoka klabuni hapo na anataka kuonesha kuwa yeye bado ni muhimu katima mkataba mpya atakaopewa
Sagna mwenye umri wa miaka 30 amaebakisha miezi 12 katika mkataba wake na amepata ofa kutoka klabu za Paris Saint Germain, Anzhi na baadhi ya klabu za mashariki ya kati.
“Nafurahia kucheza katika klabu ya Asernal. Naipenda klabu yangu, natoa mchango wa asilimia 100 kwa klabu yangu na mara zote naifanyia vizuri. Bado nipo hapa”. Alisema Sagna.
Bado yupo yupo sana: Bacary Sagna amesema anataka kuichezea klabu yake ya Arsenal
0 comments:
Post a Comment