Friday, July 19, 2013


Na Baraka Mpenja 
 Ukisia puuu! Ujue limelipuka! Maafande wa Ruvu Shooting wenye makazi yao katika dimba la Mabatini,  Mlandizi mkoani Pwani wameendeleza moto wao wa usajili baada ya kumsainisha aliyekuwa beki wa kushoto wa mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, “kwalalumpa Malysia”, Dar Young Africans, kijana mtaalamu, mwenyeji wa Mbeya, Stephano Mwasyika.
Akizungumza na MATUKIO DUNIANI asubuhi hii, afisa habari wa klabu hiyo mwenye maneno mengi na tambo kibao ambaye msimu uliopita aliwahi kuiita mechi dhidi ya Afrika Lyon ya ligi kuu kuwa ni mechi ya mazoezi kujiandaa na Yanga na kuzua hasira kubwa kwa viongozi na mashabiki wa klabu ya Lyon, Masau Bwire amesema wamemsainisha Mwasyika mkataba wa miaka mwili.
“Mwasyika ni mchezaji mzuri, mwakati wa mashindano ya majeshi  kuadhimisha miaka 50 yaJKT yalifanyika jijini Dar es salaam alikuja kufanya majaribio na baada ya mwalimu Charles Boniface Mkasa kumuona, aliridhika na uwezo wake na jana amemwaga wino wa kuichezea timu yetu yenye malengo ya kutwaa ubingwa msimu ujao”. Alisema Masau.
DSC_0776Stephano Mwasyika (kushoto) wakati akiichezea klabu yake ya zamani ya Dar Young Africans
Masau alisema siku nyingi wamekuwa wakimtolea macho nyota huyo na sasa wamefurahia kumnasa, huku akitamba kuwa kuna mchezaji ambaye wanamalizana naye na siku wakiweka wazi hakuna atakayeamini kwa kitenbdo kikubwa wanachofanya.
“Kuna mchezaji tunamalizana naye, siku nikitangaza kwa kweli watu watashangaa na hawataamini, ni mchezaji mkubwa sana, subirini muona nini tutakifanya msimu ujao, cha msingi waamuzi watende haki kwani mara nyingi tumekuwa tukionewa na waamuzi bila sababu ya msingi”. Alisema Masau.
Kwa upande wa Mwasyika, ameuambia mtandao huu kwa njia ya simu akiwa jijini Mbeya kushughulikia matatizo ya kifamilia kuwa tayari amesaini Ruvu Shooting na kuachana na magumashi ya timu yake ya Yanga.
yANGA (3)
Mwasyika ambaye aliwahi kueleza kupitia mtandao huu kuwa fitina za baadhi ya viongozi wa Yanga waliowahi kumtesa wakati akihitaji matibabu baada ya kuumia goti mpaka kwenda nchini India na kuachwa na maamivu makali, alisema ni nafasi yake kuonesha uwezo wake wa kucheza soka kwani bado ana uwezo wa  hali ya juu.
“Mpira ni popote pale, soka ni kazi yangu rasmi, sehemu yoyote yenye maslahi nakaa na kucheza, lakini cha msingi lazima Yanga wanimalizie haki zangu za msingi kwani bado nawadai. Kwasasa  mashabiki wangu wajue kuwa ni mchezaji mpya wa Shooting kwa mkataba wa miaka miwili na chini ya Mkwasa nadhani mambo yatakwenda vizuri”. Alisema.
Mwasyika alisema jumanne ya wiki ijayo atarejea jijini Dar es salaam tayari kwa kujiunga na wapiga kwata hao wa jeshi la kujenga Taifa ambao kwa sasa wapo kambini kujiwinda na msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao unaotarajiwa kuanza kushika kasi Agosti 24 mwaka huu.
Siku chache baada ya ligi kuu msimu uliopita kumalizika, mtandao huu ulifanya mahojiano na Mwasyika ambapo moja ya swali kubwa lilikuwa hivi: msimu uliopita ni timu gani zilikuvutia?. Jibu lake alitaja Ruvu Shooting na kuisifu kwa soka lake, sasa ameshajiunga nao, tusubiri kuona atafanya nini.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video