Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Manchester City imemaliza vibaya ziara yake nchini Afrika kusini baada ya jana kufungwa mabao 2-1 na klabu inayocheza ligi kuu soka nchini Afrika kusini ya Amazulu, mjini Durban
City wakiwa bila kocha wao mkuu, Pellegrini, mchezo huo ulipigwa katika dimba la Moses Mabidha ambao City walishinda kuonesha makali yao yaliyozoeleka wakiwa nchini England, na bao la kuwazamisha lilipatikana dakika za lala kwa buriani baada ya Amazulu kupata mkwaju wa penati.
Hiyo ni mechi ya pili tangu wawasili nchini Afrika kusini kufanya ziara ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England, na jumapilli ya wiki iliyopita walifungwa mabao 2-0 na SuperSports jijini Pretoria, lakini kocha wao Manuel Pellegrini alikuwa na mambo yake baada ya kukwea pipa kueleka Chile kutokana na matatizo ya kifamilia.

Nyavu zikifunguliwa : Bongani Ndulula wa AmaZulu akifunga bao la kwanza baada ya timu yake kuilaza Manchester City mabao 2-1
VIKOSI
AmaZulu: Kapini; Macala, Teyise, Msekeli, Hlanti; Madondo, Madubanya, Manqana, Zondi, Dlamini; Ndulula.
Subs: Mathibe, Zikalala, Mwedihanga, Nyadombo, Van Heerden, Cele, Issah, Mthiyane, Nsele, Manoka, Dlamini, Ngcobo.
Goals: Ndulula 20, Van Heerden pen 87
Man City: Hart (Pantilimon 63); Richards (Zabaleta 46), Kompany (Garcia 46), Nastasic (Lescott 69), Kolarov; (Boyata 75) Milner (Razak 75), Toure (Rodwell 46), Fernandinho (Barry 69), Sinclair; Dzeko (Nimely 75), Nasri (Suarez 69).
Subs not used: Huws.
Goal: Milner 26
‘Kocha wetu amerudi kwao kutokana na matatizo ya kifamilia. Tuna amini atajiunga nasi mjini Hong Kong jumanne ya wiki ijayo, lakini hatuna uhakika” Alisema kocha msaidizi wa City bwana, Brian Kidd.

Wakisawazisha: James Milner baada ya kuisawazishia klabu yake ya Manchester City






0 comments:
Post a Comment