Monday, July 22, 2013


998356_548077495250445_1818163755_n
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Siku zazidi kuyoyoma kuelekea mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani, CHAN baina ya Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa stars dhidi ya Uganda, “The Cranes”, mchezo utakaopigwa katika dimba la Nelson Mandela, Namboole, nje kidogo ya jiji la Kampala.
Mechi hiyo namba 38 itakayofanyika julai 27 saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika mashariki, Stars wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 jijini Dar es salaam julai 13 na sasa itahitaji ushindi wa zaidi ya bao moja ili kufuzu fainali za CHAN.
Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Boniface Wambura amezungumza naFULLSHANGWE na kusema kuwa kambi ya Taifa Stars inaendelea barabra CCM Kirumba jijini Mwanza, na bahati nzuri morali kwa wachezaji inazidi kupanda.
“Kambi ya Stars inaendelea vizuri hapa jijini Mwanza, Kocha Kim Poulsen anafanya kazi kubwa ya kuwafua vijana wake kwa ajili ya mchezo huo, na mara kadhaa amekuwa akikaa na wachezaji wake na kuwajenga kisaikolojia kuwa wataweza kushinda nchini Uganda”. Alisema Wambura.
Wambura alisema kihistoria si mara ya kwanza kwa Stars kufungwa nyumbani na ikaenda kushinda ugenini, kwa maana hiyo nafasi ya kwenda CHAN nchini Afrika Kusini mwakani bado ipo kutokana na mazoezi mazuri yanayoendelea CCM Kirumba.
Kuhusu kiungo mtaalamu mwenye kiwango cha juu muda wote, Salum Abubakar “Sure Boy”, Wambura alisema madaktari wa timu wanaendelea kumtibu kwa umakini mkubwa na majeruhi yake  ni ya kawaida tu.
“Sure Boy alikuwa majeruhi, lakini timu ya matatibu wetu inamfanyia huduma nzuri na tunaamini atacheza mchezo huo nchini Uganda. Niweke sawa kuwa majeruhi yake hayakuwa makubwa sana”. Alisema Wambura.
Afisa habari huyo alisema timu hiyo itaondoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza saa 7.25 mchana kwa ndege ya PrecisionAir, na inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 10.15 jioni
Wakati huo huo shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Madagascar kuchezesha mechi hiyo.
1Waamuzi wataongozwa na Kanoso Abdoul Ohabee wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Andirvoavonjy Pierre Jean Eric. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Jinoro Velomanana Ferdinand huku Andriamiharisoa Hubert Marie Bruno akiwa mwamuzi wa mezani (fourth official).
Kamishna wa mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya mwisho kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa 

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video