Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mshambuliaji hatari wa Liverpool, Luis Suarez anatarajia kuichezea klabu yake kwa mara ya kwanza katika mchezo wa pili wa maandalizi ya ligi kuu soka nchini England mjini Melbournekeshokutwa tangu afanye kitendo kibaya cha kumng`ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic.
Suarez aliwasili Australia jumamosi ya wiki iliyopita akitokea mapumzikoni na sasa yupo na kikosi cha Brendan Rodgers, huku kocha huyo akisisitiza kuwa nyota wake atabakia Anfield.
Mechi hiyo ya kesho kutwa meneja wa majogoo wa jiji anatarajia kumpanga mshambuliaji huyo raia wa Uruguay ambaye hajatulia kwa sasa klabuni kuongoza safu ya ushambulizi dhidi ya Melbourne Victory katika dimba la MCG, lakini kabla ya mechi hiyo Rodgers anatarajia kuzungumza na Suarez kuhusu hatima yake ya baadaye klabuni hapo.
Suarez ambaye amekuwa gumzo katika hekaheka za usajili, akihusishwa na mpango wa kutaka kuihama klabu yake, huku Arsenal wakiwa mstari wa mbele kuitaka saini yake kwa ada ya uhamisho ya pauni 40, lakini hali aliyoionesha wakati akiwasili Austaria inabadili mawazo ya wengi hususani baada ya kukataa kuongea na waandishi wa habari juu ya maisha yake ya msimu ujao.
Wakati huo huo kocha wake Rodgers alisisitiza kuwa matarajio yake ni kuwa Saurez atabakia Anfield msimu ujao na klabu yake haina mpango wa kumuuza.
Kuelekea mchezo wa kesho kutwa dhidi ya Melbourne Victory, tayari mpaka sasa tiketi 90,000 zimeshauzwa




Suarez alifanya mazoezi AMMI leo hii na kuonekana ana morali kubwa katika kibarua cheka katika klabu ya Liverpool




0 comments:
Post a Comment