Kibadeni alisema jana, licha ya usajili kufanyika, bado anahitaji beki wa kati wa kusaidia timu hiyo kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu ujao.
Alisema, anaamini kama atapatikana beki wa kiwango anachokitaka, timu hiyo itakuwa imekamilika, hivyo anaamini Kamati ya Usajili italifanyia kazi kwa masilahi ya timu hiyo.
“Naomba Kamati ya Usajili ifanye juhudi za kumpata beki wa kati wa kuongeza nguvu katika kikosi hiki kinachozidi kuimarika,” alisema Kibadeni.
Aidha, Kibadeni alisema anamhitaji beki huyo awe na umbile kubwa na urefu kama nyota Mzambia, Felix Sunzu.
Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans-Pope alisema wameshapata ombi la Kibadeni na wanalifanyia kazi.
“Tumemsikia na tunafanyia kazi ushauri wa benchi la ufundi na tutalifanyia kazi ombi lake kwa masilahi ya timu,” alisema Pope.
0 comments:
Post a Comment