MWANASOKA bora wa dunia, Lionel Messi ametembelea akademi ya Aspire nchini Senegal ambako kuna mchezaji mmoja chipukizi kutoka Tanzania, Orgenes Molel.
Na
akiwa huko, amesema anaamini kocha mpinzani wake wa zamani, Jose
Mourinho atapata mafanikio Chelsea na ameweka wazi, Mreno huyo ni 'bonge
la kocha'.
Mourinho amerejea Chelsea baada ya kumaliza kuitumikia Real Madrid mwishoni mwa msimu uliopita.
Kocha
huyo wa zamani wa Porto na Inter Milan alikuwa maarufu Hispania
kutokana na kukuza upinzani wa Real na Barcelona katika kipindi
alichokuwa akifanya kazi Madrid.

Mtu kati: Lionel Messi alikuwas Senegal kutembelea akademi ya Aspire Academy

Mapokezi makubwa: Messi amepata mapokezi makubwa Senegal alipokwenda katika kampeni ya kupiga vita Malaria kwa nchi za Afrika


Mafanikio: Mourinho amechukua nafasi ya Rafa Benitez Chelsea

Carlo Ancelotti (katikati) amerithi mikoba ya Mourinho Madrid
0 comments:
Post a Comment