
Frank Pangani, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Taasisi ya Michezo ya Nationwide Entertainment Center (NEC), alisema jana kuwa Yanga itaondoka jijini Dar es Salaam, Julai5.
Alisema wakiwa Mwanza, watacheza na mabingwa wa Ligi Kuu ya Uganda, Kampala City Council (KCC) katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo kabla ya Julai 7 kurudiana nao katika Uwanja wa CC, Kambarage mjini Shinyanga.
“Mwaka jana tulifanya kwa Simba waliokuwa mabingwa na safari hii ni Yanga,” alisema Pangani.
Baada ya kumaliza ziara hiyo ambayo itaenda sambamba na utembezaji wa Kombe la Ligi Kuu, Julai 11 watakuwa Tabora ambapo watacheza mechi ya kirafiki.
Naye Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kaziguto alisema watafanya juu chini ziara hiyo isiingiliane na kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars ambayo itaingia kambini Julai 3, kujiandaa dhidi ya Uganda.
Aidha, Kaziguto alisema hawana mpango wa kumsajili kipa wa Simba, Juma Kaseja, aliyetupiwa virago Msimbazi.
Aliongeza kuwa licha ya klabu yao kuwa na nyota 10, si jukumu lao kuweka wazi mazungumzo yao.
0 comments:
Post a Comment