Na Baraka Mpenja
Mabingwa wa kombe la Kagame na Vinara
wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga ya Dar es salaam yenye makazi
yake mitaa ya Twiga na Jangwani kesho
inatarajia kushusha daluga zake za wanaume kumi na mmoja dhidi ya maafande wa jeshi la kujenga taifa
kutoka jijini Arusha “Geneva ya Afrika”, klabu ya JKT Oljoro, mchezo
utakaopigwa uwanja wa taifa majira ya saa kumi kamili jioni.
Akizungumza na matandao huu, Afisa
habari wa klabu hiyo “Kwalalumpa Malysia”, Baraka Kizuguto amesema mchezo huo ni muhimu sana kwao ingawa
mabadiliko ya ratiba yamewaathiri kutokana na maandalizi waliyofanya kucheza aprili
10 mwaka huu na sio kesho.
Kizuguto alisema licha ya kuwepo
changamoto kama hizo, wao wanaheshimu kila mchezo huku wakihitaji ushindi na
kuweza kumaliza ligi msimu huu wakiwa mabingwa wa taji hilo.
“Tumejipanga kushindana katika uwanja
wa nyumbani dhidi ya timu ngumu ya JKT Oljoro, tunajua fika kuwa maafande hawa
ni wagumu sana, lakini tumefanya maandalizi makubwa sana kuhakikisha tunapata
matokeo ya ushindi”. Alisema Baraka.
Akizungumzia afya za wachezaji wao,
Kizuguto alisisitiza kuwa wachezaji wote wapo kambini wakiwa salama na wanaendelea
na mazoezi ya mwisho mwisho kuwakabili Oljoro hapo kesho.
“Yanga haina majeruhi ambaye yupo
hatarini kuukosa mchezo wa kesho, kilichobaki ni kusubiri muda ufike ili
tukacheze mechi hiyo”. Alisema Kizuguto.
Pia afisa habari huyo aliwataka
wapenzi na wanachama wa Yanga kufika kwa wingi uwanja wa taifa ili kuwapa nguvu
wachezaji wao wenye lengo la kuwapatia zawadi ya ubingwa msimu huu.
Wakati Yanga wakijinasibu kuwa wako
barabara, nao Oljoro wamejibu mapigo kuwa kesho ni kutafuta heshima mbele ya
vinara wa ligi hiyo na wakongwe wa soka la Tanzania.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo Riziki
Shawa, amesema kuwa wao wameshapanga
makombora ya kuwamaliza Yanga wenye ngebe ya kutwaa ubingwa msimu huu.
“Kinachowabeba Yanga kwa sasa ni
bahati tu, timu yao ni ya kawaida sana, sisi tumejipanga kuwaadabisha katika
uwanja bora wa taifa mbele ya umati wa mashabiki wao”. Alijigamba Shawa.
Shawa alisema klabu hiyo tayari ipo
jijini Dar es salaam tayari kwa kuwavaa wanajangwani hapo kesho.
Yanga kwa sasa wapo kileleni
wakijikusanyia pointi 49 kibindoni, huku Azam fc wakiwa nyuma yao kwa pointi 46
lakini Azam wamecheza mechi moja zaidi.
Kama Yanga watashinda kesho wataweka
pengo la pointi 6 huku wakisubiri mchezo wa jumapili kati ya mabingwa watetezi
Simba dhidi ya wana lambalamba Azam fc mchezo utakaopigwa uwanja wa taifa.
3 comments:
JKT Oljoro,wawakilishi pekee wa A-town,ama ukipenda Genever ya Africa, nawatakia kila la heri,waadabisheni hao YANGA!
oljoro wakimbizeni yanga! hawana lolote.
good news, thanks!
Post a Comment