
Na Baraka Mpenja
Usaili wa wachezaji watakaoshiriki michuano
ya vijana chini ya umri wa miaka 12 na 14 manispaa ya Ilala inayotarajiwa
kuanza kutimua vumbi mei mosi mwaka huu umepangwa kufanyika aprili 13 na 14
mwaka huu majira ya saa sita mchana katika uwanja wa karume jijini Dar es
salaam.
Akizungumza na Mtandao huu mwenyeki
wa chama cha soka la vijana wilaya ya Ilala (IDYOSA), Father Edwirn Mloka amesema
usaili huo wenye lengo la kupata umri sahihi kwa timu shiriki utajumuisha timu
11 za wilayani hapo.
Mloka alisema jumamosi ya Aprili 13, usaili
utafanyika kwa timu za Tabata Rangers, Home Team, Vumbua vipaji, New Team,
Muheza Kids na Tabata Twiga.
Siku inayofauta aprili 14 timu za
Kinota, Makoba, Sinepa Academy, Elimu Kids na Lili Boys zitafanyiwa usaili huo.
Mwenyekiti huyo wa IDYOSA,
alisisitiza kuwa viongozi wa timu hizo wanatakiwa kufika bila kukosa na muda
lazima uzingatiwe kama ulivyopangwa.
“Soka la vijana linatakiwa kuzingatia
nidhamu, kuchelewa ni moja kati ya makosa ya utovu wa nidhamu, kama wachezaji
watachelewa kufika kwa sababu ya uzembe wa viongozi, hakika watachukuliwa hatua
za kinidhamu”. Alisema Mloka.
Mloka alisema soka la sasa linahitaji
kuwezekeza kwa vijana wadogo, hivyo wilaya ya Ilala inataka kuwa mfano wa
kuigwa kwa wilaya zote nchini Tanzania.
Kiongozi huyo mwenye hulka ya
kuendesha soka la vijana, aliongeza kuwa lazima wadau wa soka, makampuni
mbalimbali yakubali kuwekeza katika soka la vijana kwani ndio msingi wa taifa
lolote.
“Mara nyingi tunahangaika kutafuta
misaada wakati watu wenye uwezo wanajitokeza kudhamini timu za ligi kuu, lazima
watambue kuwa msingi wa soka kwa sasa ni vijana wadogo ambao siku zote
hufundishika kirahisi kuliko wakongwe”. Aliongeza Mloka.
Mbali na zoezi la usaili, Mloka
alisema chama chake kimepata mwaliko wa kupelekea timu ya soka mkoani Tabora
mwezi juni mwaka huu ili kudumisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu wa
kuongoza soka la makinda kwa wilaya hizo mbili.
Mloka alisisitiza kuwa mashindano
yanayoanza mwezi ujao yatasaidia kupata timu ya kusafiri mpaka kwa wanyamwezi
wa Tabora, hivyo kila timu shiriki iwaandae vijana wake kushindana na kutoa
wachezaji wa kwenda huko.
0 comments:
Post a Comment