
Uswizi
Nahodha wa watukutu wa London,
klabu ya Tottenham Hospur, Michael Dawson amesema timu yake inaweza kufanya
maajabu na kuwafumua wapinzani wao Basel ya Uswisi mchezo wa ligi ya Uropa
unaotarajia kupigwa usiku wa leo katika dimba la mtakatifu Jakob-park na hatimaye
kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Nyota huyo amesema kuwa kuna watu
wanafikiri kuwa matokeo ya sare ya 2-2 wiki mbili zilizopita jijini London
yamewaathiri sana na hawana uwezo wa kuyapindua, lakini wao wanajiamini na
wanaweza kushinda na kuwaduwaza mashabiki wataofurika uwanjani leo.
Nyota huyo amewaondoa hofu na
kuwajengea imani ya ushindi mashabiki wa klabu hiyo ambayo katika dimba lake la
nyumbani la White Hart Lane walianzia nyuma na kusawazisha mabao mawili baada
ya kufungwa mapema.
Akizungumzia mkakati wake wa
kubakia klabuni hapo katika dirisha dogo la usajili, Dawson, amesema ataendelea
kupambana kubakia ingawa kocha wake Andre Villas-Boas AVB ameonesha nia ya
kumuuza katika klabu ya QPR majira ya joto.
Nyota huyo ambaye amepata namba
katika kikosi cha kwanza baada ya Younes Kaboul kukumbwa na majeruhi amesema
bado anaamini kuwa ataisaidia timu na kufikia mafanikio makubwa.
“Ningekuwa nimeshaondoka Spurs,
lakini kamwe sikati tamaa, leo hii ni furaha kubwa kwang kuwaongoza vijana na
nitajisikia faraja sana endapo tutafanikiwa, najua haitakuwa kazi nyepesi
lakini lazima mtu uwe na imani”. Amesema Dawson.
Spurs itamkosa mpachika mabao
wake Gareth Bale ambaye ni majeruhi, lakini wanamtegemea sana Mtogo Emmanuel
Adebayor ambaye AVB anaamini atawaongozwa vyema mbele ya Basel.

0 comments:
Post a Comment