Monday, April 15, 2013


kibaden
Kibadeni akifanya kazi yake
Na Baraka Mpenja
Wakata miwa wa kagera sugar wanajiandaa na kibarua kigumu cha kuwakabili wapinzania wao wa kanda ya ziwa Toto Africa kesho kutwa katika dimba lao la nyumbani, Kaitaba mjini Bukoba.
Mzunguko wa kwanza Kagera sugar waliwatungua Toto mabao 2-1 katika uwanja wa CCM Kirumba na sasa wanakutana tena bukoba kuonshana shughuli pevu.
Kocha mkuu wa klabu ya Kagera sugar, Abdallah Kibadeni “King Mputa” amesema leo hii asubuhi wameanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo.
“Tumepumzika kwa siku nyingi lakini leo hii vijana wamefika uwanjani ili kuwekana sawa kabla ya kuwavaa ndugu zetu Toto wenye nia ya kukwepa mkasi wa kushuka daraja”. Alisema Kibadeni.
Kocha huyo aliyewahi Kutamba na simba akicheza winga miaka ya sabini pia kuwa kocha wake, aliongeza kuwa mchezo huo ni mgumu sana kutokana na ukweli kwamba wapinzania wao wanausaka ushindi kwa nguvu zote, lakini vijana wake wanajengwa kupambana kwa mbinu nyingi za kiufundi ili kuwadhibiti wana kishamapanda.
Kibadeni alisema hesabu zake ni kupata nafasi nzuri katika msimamo ili kupata angalau nafasi ya kucheza michauno ya kimataifa hivyo mchezo wa keshokutwa ni lazima kushindi ili kuongeza kasi yake zaidi.
“Tupo nafasi ya tatu kwa pointi 37, simba wanakuja nyuma yetu, najua wanapambana kweli , lakini sisi tunajipanga kuhakikisha hatutoki pale tulipo labda tusonge mbele zaidi”. Alisisitiza kibadeni.
Akizungumzia hali ya ligi hususani dakika hizi za lala kwa buriani, Kibadeni alisema ligi kuu imekuwa ngumu zaidi kwani kila timu inaonekana kujipanga zaidi ili kujiweka mazingira mazuri.
“Hakika hadi dua za mashabiki kwa sasa zinahusika sana, wana Kagera watuunge mkono ngwe hii ya lala salama, kikubwa wasiliachie kampuni pekee kwani hata wao wanatakiwa kutusaidia hata kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani”. Alisema King Kibadeni.
 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video