Timu ya bluu-Tanzania:
Khenry
Sadallah(26) na Abubakari Mohamed(19) kutoka Dar-es-Salaam watashiriki
katika sehemu ijayo. Harry atakuwa kichwa cha timu ambaye ni mshabiki
wa AC Milan wakati Abubakari ambaye ni mwanafunzi na mshabiki wa
Manchester United ataonesha uwezo wake wa kucheza mpir
Timu nyekundu-Kenya:
- Ken Muturi (26) na Chris Mwamgi (19) wote kutoka Nairobi wanamatumaini makubwa yakuwa timu ya mwisho kuingia kwenye mashindano ya Pan African. Ken ni mfanyabiashara kwa njia ya mtandao, ni mpenzi wa mpira wa miguu ambapo atakuwa kichwa cha timu wakati Chris ambaye ni mchezaji wa Springland FC ataonesha kipaji chake cha mpira wa miguu.
Timu ya kijani-Uganda
- Mfanyabiashara Ian Ford(24) na mwanafunzi wa uchumi Herbet Odipio(23) kutoka Kampala ni mashabiki wa Manchester United watashiriki katika kipindi kijacho cha mashindano Guinness Football Challenge. Ian atakuwa kichwa cha timu wakati Herbet ataonesha uwezo wake wa kusakata kabumbu.
Timu nyeusi-Uganda:
Edward
Lyukamuzi(23) na Timothy Nimungu(22) kutoka Kampala ni timu ya pili
kutoka Uganda watashiriki kipindi cha 5 cha mashindano haya. Edward ni
mtaalamu wa Teknolojia ya mawasiliano ndiye kichwa cha timu wakati
Timothy ambaye ni mtaalamu wa masoko atonesha uwezo wake wa kucheza
soka.
April
10, 2013, Dar es Salaam; Jumatano iliyopita katika sehemu ya nne
kupitia televisheni za ITV na Clouds TV, mashindano ya GUINNESS®
FOOTBALL CHALLENGE™ yalikuwa na ushindani mkubwa lakini washiriki
kutoka Kenya Enphatus Nyambura na Samuel Papa waliweza kumudu vishindo
na kufanikiwa kuwa timu ya tatu kutoka Kenya kuingia katika hatua ya
Pan- Africa, baada ya kuwapiga chini timu za Tanzania na Uganda.
Katika kipindi hiki cha nne washiriki walijitahidi kufanya vizuri katika
kuonesha uwezo wao wa kuchezea mpira na kujipatia alama nyingi japo
walishindwa kujibu maswali kwa ufasaha.Washiriki kutoka Kenya
walifanikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya kulenga ukuta wa pesa wa
Guinness ambapo walijishindia dola kimarekani 1,500.
Enphatus
na Samwel wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo
ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia kitita cha
fedha za kimarekani hadi kufikia dola 250,000. Washiriki bora
watakwenda kukutana uso kwa uso na mashabiki wa soka kutoka nchi za
Cameroon,Ghana,Tanzania, Kenya, na Uganda ili atakayeonesha ufahamu na
ujuzi zaidi wa soka atavishwa taji la ubingwa wa` Pan-African’.
GUINNESS
FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni
ya kimataifa ya Endemol. Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika
televisheni za ITV na clouds TV. Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV
kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku ambapo Clouds TV
itarusha kipindi hicho saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .
Katika
kipindi cha tano cha mashindano haya yatakayooneshwa na vituo vya
televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne ndizo zitakua uwanjani
kuchuana vikali, ni timu ipi itakayowapiga chini wengine na kuingia
katika hatua ya Pan Africa? Majibu yote yatapatikana Jumatano hii.
Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness Football Challenge barani Afrika
wanakumbushwa kwamba, wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa njia ya
mtandao. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika
tovuti ya m.guinnessvip.com.
Pia GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook ambayo ni www.facebook.com/guinnesskenya,
Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kufuatilia ukurasa huu
‘like’ na utakuwa unapata habari zote zinazohusu mchezo huu.
GUINNESS
FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na
kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia
kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV
kila siku ya Jumatano usiku.
Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.
*Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na nane. Tafadhali Kunywa kistarabu.
0 comments:
Post a Comment