Na Baraka Mpenja
Baada ya kufuzu
raundi ya tatu ya kombe la shirikisho na kupangiwa timu ya jeshi la Morroco FAR
Rabat, mabingwa mara mbili wa taji la mapinduzi na makamu bingwa wa kombe la
Kagame, klabu ya Azam fc yenye makazi yake Mbade Chamazi nje kidpgo ya jiji la
Dar es salaam, sasa imehamishia majeshi yake katika mchezo wa ligi kuu soka
Tanzania bara dhidi ya Africa Lyon keshokutwa uwanja wa chamazi.
Akizungumza kwa
kujiamini, afisa habari wa klabu hiyo,
Jafar Idd Maganga amesema kamwe hawadharau mchezo wowote na ndio maana
wanaendelea kujifua ili kuwakabili Lyon
wanaopambana kufa na kupona kukwepa panga la kurejea ligi daraja la kwanza.
“Africa Lyon wapo
makini na hawajashuka daraja, bado wapo kwenye ushindani mkubwa, tunalitambua
hilo na ndio maana tunaandaa kikosi cha kwanza kwa ajili ya mchezo huo muhimu
kwetu, tukipata pointi tatu zitatusaidia kupata nafasi nzuri katika msimamo na
kuwakilisha taifa kimataifa mwakani”. Alisema Idd.
Afisa habari huyo
aliongeza kuwa mpaka sasa wachezaji wote ni wazima, hivyo wataingia kwa nguvu
zote kuwakabili wapinzani wao katika dimba la nyumbani, Chamazi Complex maaneo
ya Mbande.
Akizungumzia hali
halisi ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu, Idd alisema ushindani ni
mkubwa na ndio maana kila unapoingia uwanjani, unatakiwa kutumia akili nyingi
kupata matokeo ya ushindi.
“Kabla ya kuvaana na
Barrack YC, tulicheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting na kuwafunga
1-0 katika uwanja wao, tulikabiliana na changamoto kubwa kutokana na ubora wao,
lakini keshokutwa tunahitaji sana pointi tatu na lazima zipatikane kulingana na
uwezo wetu kwa sasa”. Alijigamba Idd.

Wakati Azam fc
wakijipanga vilivyo kuwaadhibu Lyon, nao kwa upande wao wamesema maandalizi
yanakwenda vizuri na wanahitaji ushindi katika mchezo huo.
Mkurugenzi wa ufundi
wa klabu hiyo, Mkenya, Charles Otieno alisema wanang`ang`a kusalia ligi kuu msimu
huu na ushindi waliopata mechi mbili zilizopita umewapa nguvu kubwa, hivyo Azam
lazima wajipange kweli kweli.
“Tatizo la klabu yetu
ni safu ya ushambuliaji, tunapata nafasi nyingi lakini huwa tunashindwa
kuzitumia, lakini kwa sasa tumefanya mazoezi ya kufunga na tunaamini siku hiyo
tutafanya vizuri mbele ya wapinzani wetu”. Alisema Otieno.
Azam fc wataingia
uwanjani wakiwa na ndoto za kutwaa ubingwa msimu huu wakiwa na pointi 43 nyuma
ya vinara Yanga wenye pointi 49.
Afrika Lyon wapo
nafasi ya 12 wakiwa na mzigo wa poniti 19 wakipambana kwa nguvu zote kusalia michuano
ya ligi kuu soka Tanzania bara.
![]() |
AFRICA LYON |
0 comments:
Post a Comment