Mabingwa mara mbili wa kombe la mapinduzi, makamu bingwa wa ligi kuu bara na Kome la kagame, klabu ya Azam fc yenye makazi yake Pande Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam, imezitaka klabu za ligi kuu Tanzania bara kufanya maandalizi ya muda mrefu kabla ya kushiriki michuano hiyo ili kupata matokeo mazuri yakuwafurahisha wanachama na mashabiki hayo.
BENCHI LA UFUNDI LA AZAM FC |
Afisa habari wa klabu hiyo Jafar Idd Mganga amesema wao kama Azam walijitahidi kuweka kambi mapema na kuzingatia maombi ya waalimu wao na ndio maana walikwenda nchini Kongo, Kenya na kushiriki michuano ya mapinduzi na kusababisha kikosi chao kujengeka zaidi.
Idd alisema soka ni maandalizi, jinsi utakavyoaanda timu yako ndivyo utakavyovuna matundu ya uwanjani kwani mababu zetu waliwahi kusema "ukipanda matembele utavuna matembele".
Pia Azam alizitaka klabu kufanya usajili mzuri ili zipate wachezaji watakaohimili mikikimikiki ya ligi ya "premia" Tanzania ambayo inaonekana kutawaliwa na timu tatu yaani Simba (wazee wa Oman), Yanga (wazee wa Uturuki) na Azam fc (wazee wa Kongo na Kenya).
Kuhusu baadhi ya timu kupanga matokeo ya uwanja, Idd amesema Azam fc daima hawana tabia hiyo ila kinachowafanya wapate matokeo mazuri ni maandalizi mazuri na usajili wa wachezaji unaozingatia viwango vyao na sio majina.
Wana lambalamba hao jana waliibamiza Toto Africa ya mwanza kwa jumla ya mabao 3-2 katika mchezo wa hatua ya 15 ya ligi kuu Tanzania bara.
Kabla ya mchezo huo wa jana Azam ilishinda mchezo wa kwanza januari 26 dhidi ya kagera Sugar kwa jumla ya mabao 3-1 na sasa ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 30 nyuma ya Yanga wenye pointi 32 katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo.
Simba wapo katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 26 huku wakijiandaa na mchezo wao wa jumapili ya wiki hii dhidi ya maafande wa jeshi la kujenga taifa Ruvu shooting ya mkoani Pwani, huku Yanga wakijandaa kucheza dhidi ya Mtibwa sugar jumamosi ya wiki hii katika uwanja wa taifa.
Katikam mchezo wa kwanza mzunguko wa kwanza Mtibwa waliifunga Yanga 3-0 hivyo mechi hiyo ni ya kulipa kisasa kwa wazee hao wa Uturuki.
0 comments:
Post a Comment