Thursday, January 31, 2013


Na Baraka Adson
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).

Katika kikosi hicho wachezaji wengi wametoka timu tatu tu Simba, Azam fc, Yanga na Mtibwa sugar, wakati timu zilizosalia hazijatoa mchezaji hata mmoja.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.

“Itakuwa mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.

“Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.

Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam).

Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba).

Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Ukiangalia kikosi cha Kim Paulsen bado kinaonesha klabu tatu za ligi kuu bara Yanga, Simba na Azam fc kutawala timu ya taifa.
Kikosi cha awamu hii wachezaji wawili tu ndio wametoka nje ya timu tatu bora za ligi kama inavyoonekana hapo chini.

AZAM
Mwadini Ally, Aishi Manula, Erasto Nyoni, Agrey Morris, salum Abubakar, Hamis Mcha (wachezaji 6 kutoka Azam fc).
SIMBA
Juma kaseja, Masud Nassoro Cholo, Amri Kiembe, Mrisho Ngasa, Mwinyi kazimoto na shomari Kapombe. (wachezaji 6 kutoka simba).
YANGA
Kelvin Yondan, Nadir Haroub “canavaro”, Simon Msuva, Athman Idd Chuji, na Frank Domayo.(wachezaji 5).
Mtibwa sugar
Issa Rashid na Shaban Nditi. (wachezaji 2).
TP MAZEMBE
Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata. (Wachezaji 2).

Timu tatu tu ndio zimeunda kikosi cha stars, je timu nyingine ambazo zinacheza ligi kuu hazina wachezaji wazuri?

Prisons, JKT Ruvu, Ruvu shooting, Kagera sugar, coastal union, Polisi Morogoro, JKT Oljoro, afrika Lyon.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video